Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Lenga nyota ili ukizikosa uupate mwezi asema Alinda Mashiku mwanasayansi mhandisi wa NASA

Dkt. Alinda Mashiku, Meneja wa Mpango wa Uchambuzi wa Hatari za Migongano Angani (CARA) katika Kituo cha Kitaifa cha masuala ya Anga za mbali cha NASA Goddard, Maryland nchini Marekani.

Watu hawakuitazama nguvu ya uvutano wa dunia na kusema hatuwezi kwenda

Dkt. Alinda Mashiku , Mhandisi NASA

Habari za Umoja wa Mataifa Alinda Mashiku ni mhandisi wa anga na mwanasayansi aliyefanikiwa anayeshughulikia kazi kama Meneja wa Programu ya Programu ya Uchambuzi wa Hatari ya Kukutana (Conjunction Assessment Risk Analysis - CARA) ya NASA katika Kituo cha Nafasi cha NASA Goddard, ambapo anaongoza jitihada za kulinda satelaiti kutoka au

Lenga nyota ili ukizikosa uupate mwezi asema Alinda Mashiku mwanasayansi mhandisi wa NASA

Na Anold Kayanda
Wanawake

Anold Kayanda wa Idhaa ya Umoja anazungumza na Dkt. Alinda Mashiku, Mhandisi wa masuala ya anga katika moja ya Vituo vya masuala ya anga za mbali nchini Marekani, NASA. Kwa kuzingatia kuwa Umoja wa Mataifa unapigia chepuo wasichana na wanawake kupata fursa katika sayansi na teknolojia, swali la kwanza la Anold Kayanda kwa Alinda Mashiku ni ameipokeaje hatua ya hivi karibuni ambapo kwa mara ya kwanza mwanamke Christina Coch ameshiriki katika timu ya wana-anga waliosafiri na kufanikiwa kuuzunguka mwezi katika eneo mbali zaidi katika anga ya mbali ambako kulikuwa hakujawahi kufikiwa na  wanadamu?