Fahamu jinsi ECSA-HC inavyosongesha diplomasia ya kisayansi
Mkurugenzi Mkuu wa Jumuiya ya Afya ya nchi za Mashariki, Kati na Kusini mwa Afrika, ECSA-HC akizungumza na Idhaa ya Umoja wa Mataifa, New York, Marekani.
Fahamu jinsi ECSA-HC inavyosongesha diplomasia ya kisayansi
Afya
Mkurugenzi Mkuu wa Jumuiya ya Afya ya Mashariki, Kati na Kusini mwa Afrika, ECSA-HC, Dkt. Ntuli Kapologwe akihojiwa na Assumpta Massoi wa Idhaa hii anaelezea mantiki ya jumuiya hiyo kuandaa kwa ushirikiano na serikali ya Tanzania mkutano wa kusongesha diplomasia ya kisayansi, mkutano unaofanyika kando ya mjadala mkuu wa mkutano wa 80 wa Baraza Kuu la UN, UNGA80 kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa New York, Marekani Septemba 24, 2025.