Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ukame ukisogea wafugaji uzeni mifugo kuepusha hasara - Dkt. Mutungi

Mwanamke akilisha mifugo yake huko jimboni Somali nchini Ethiopia

“Kwa wafugaji napenda kuwahimiza ya kwamba, wanapoona ukame umeanza na unaweza kuwa hatari basi wauze mifugo yao mapema waweke pesa mfukoni kwa sababu mifugo inakufa lakini fedha hazifi zinaweza kumsaidia baadaye kujikimu kimaisha.”

Dkt. Paul Mutungi , Afisa wa Mashinani - FAO

© UNICEF/Mulugeta Ayene
Mwanamke akilisha mifugo yake huko jimboni Somali nchini Ethiopia

Ukame ukisogea wafugaji uzeni mifugo kuepusha hasara - Dkt. Mutungi

Msaada wa Kibinadamu

Huko Afrika Mashariki na Pembe ya Afrika ambako huko kwa kipindi kirefu sasa njaa na ukame vimekuwa tatizo kubwa. Mwezi uliopita wa Januari shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo FAO lilitoa ombi la zaidi ya dola milioni 138 za ufadhili wa dharura ili kusaidia watu milioni 1.5 walio hatarini katika jamii za vijijini huko Afrika Mashariki na Pembe ya Afrika. Kufahamu hali halisi mashinani iko vipi, Leah Mushi wa Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa amezungumza na Dokta. Paul Mutungi Afisa wa mashinani wa FAO akihusika na wafugaji katika Ukanda wa Afrika Mashariki na anaanza kwa kueleza hali ya kibinadamu ilivyo huko mashinani.