6 Oktoba 2020

Takwimu za Umoja wa Mataifa zinaonyesha kwamba bayoanuai ya dunia inaendelea kupotea na endapo hatua madhubuti hazitochukuliwa sasa basi  mustakbali wa viumbe vya dunia wakiwemo binadamu, mazingira na sayari yenyewe kwa kizazi hiki na vizazi vijavyo utakuwa njiapanda.  

Umoja wa Mataifa umeendelea kuzihimiza nchi wanachama kuzingatia suala hili ambalo ni muhimu kwa kila nyanja ya maisha ukisisitiza pia “Hatua za haraka kuchukuliwa kuhusu bayoanuai kwa ajili ya maendeleo endelevu” SDGs.  

Ili kufahamu ni kwa kiasi gani tatizo hilo ni kubwa na kwa nini ni muhimu sana kuchukua hatua kuliko wakati mwingine wowote  kulinda bayoanuai, Flora Nducha wa Idhaa hii amezungumza na Bi. Elizabeth Mrema katibu mtendaji wa mkataba wa Umoja wa Mataifa kuhusu masuala ya bayoanuai, CDB ungana nao

 

♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter