19 Septemba 2018

Ulinzi wa amani ni moja ya kazi kubwa ambazo zinatekelezwa na Umoja wa Mataifa kwani migogoro nayo inazidi kushuhudiwa katika nchi mbalimbali.

Kazi hii muhimu inayotekelezwa na Umoja wa Mataifa inahitaji ushirikiano na nchi wanachama kwani wao ndio wanachangia vikosi vya kulinda amani katika nchi wanakohitajika. Licha ya umuhimu wa wajibu huo lakini hapakosi changamoto zinazokabili nchi zinazochangia katika kufanikisha ulinzi wa amani. Moja ya nchi ambazo zinachangia walinda amani ni Tanzania ambapo hivi karibuni wamefanya mkutano wa pande mbili na Umoja huo kujadili mabadiliko na changamoto katika operesheni za ulinzi wa amani.

Meja Jenerali Alfred Fabian Kapinga ni mkuu wa operesheni na mafunzo wa jeshi la wananchi wa Tanzania (JWTZ), amezungumza na Flora Nducha wa Idhaa hii akiangazia ikiwemo mkutano wao na UM, hapa anaanza kwa kuelezea mkutano ulihusu nini? 

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud