Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Uganda yazindua kampeni ya chanjo dhidi ya kipindupindu-WHO

Dawa mpya ndiyo tumetumia

Bi. Sarah Opendi waziri wa afya wa Uganda. Picha: UM/Idhaa ya Kiswahili

Uganda yazindua kampeni ya chanjo dhidi ya kipindupindu-WHO

Afya

Kila mwaka nchini Uganda hutokea wastan wa visa1,850 vya kipindupindu na takriban vifo 45. Hii ni kwa mujibu wa waziri wa Afya wa Uganda Dkt Jane Ruth Acieng alipozungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni hiyo.

Visa vingi hutokea sehemu za Mashariki, Kaskazini na Kaskazini Magharibi mwa Uganda. Zoezi hili linadhaminiwa na  shirika la kimataifa la muungano wa chanjo ,GAVI na dawa inayotumika ya matone ndio inatumika kwa mara ya kwanza nchini Uganda.

Siraj Kalyango wa Idhaa hii amezungumza na waziri wa afya anehusika na shughuli za jumla , Dkt Sarah Opendi, kuhusu chanjo hii.