Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Utamu wa lugha ni pale inapotumiwa kwa ufasaha.

Kiwango cha matumizi ya Kiswahili kimedorora

Ken Walibora, mshairi na mwandishi wa vitabu mashuhuri kutoka Kenya. (Picha:Kwa hisani ya Ken Walibora)

Utamu wa lugha ni pale inapotumiwa kwa ufasaha.

Utamaduni na Elimu

Kiswahili kimekuwa na mchango mkubwa kwa wazungumzaji wake hususan Afrika Mashariki kikipigwa jeki na vyombo vya habari kama Radio kwa miaka mingi. Lakini sasa hali ikoje katika kukuza na kuendeleza lugha hii?  Ken Walibora ni mwana riwaya na pia amekuwa mwandishi habari akitumia lugha ya Kiswahili miaka nena miaka rudi,  Katika mahojiano ,maalum na Siraj Kalyango wa Idhaa hii amezungumzia lugha hiyo na jinsi vyombo vya habari vinavyohusika kuiendeleza.