
Yevheniya alimzaa Yehor mwezi Februari 2022. Anaeleza yeye na mume wake walitumia miezi kadhaa kuandaa nyumba yao huko Mariupol, mashariki mwa Ukriane. Walinunua nguo za watoto, gari ya mtoto kutembelea na michezo ya mtoto.
Vita ilipoanza na mlio wa kwanza wa mlipuko kusikika huko Mariupol Februari 24, mipango yao yote ya malezo na furaha kwa mtoto wao ilibadilika mara moja. Yevheniya haraka alipakia mabegi mawili moja ya familia na nyingine ya mtoto.
“Tuligundua ilikuwa hatari kukaa katika mkoa wa Donetsk na kwamba tunapaswa kuondoka haraka iwezekanavyo,” anakumbuka Yevheniya. Buti la gari letu ni dogo sana, kwa hivyo tuliweza kuchukua vitu muhimu zaidi kepe.”

Familia ilisafiri saa saba kwa gari hadi Dnipro, bila kusimama wala kupumzika. Yevheniya anasema alitambua umuhimu wa kuwa na uwezo wa kunyonyesha, kumpa mtoto wake uhakika wa chakula na ulinzi dhidi ya magonjwa hata kama ulimwengu wao ulikuwa umeanguka.
“Alikuwa na umri wa mwezi mmoja tu.” Safari yetu ilienda vizuri kwa sababu ya kunyonyesha tu.Alikuwa na maziwa ya kopo pamoja namimi, lakini pia maji kwa joto tuliyoweka kwenye chupa. Ni vigumu sana kupanga haya yote katikati ya safari, hasa wakati wa vita."
Tangu kuzuka vita nchini Ukraine, kunyonyesha kumekuwa suala muhimu kwa familia ya Yevheniya. Maziwa ya mama ndio ufunguo wa kuishi na usalama kwa mtoto wake Yehor ambaye katika maisha yake mafupi tayari ameshuhudia vita na kuwa mkimbizi ndani ya nchi yake.
“Wakati wa vita, maziwa ya mama ni kitu ambacho kinanifanya nijiamini kuwa siku zote nina kitu cha kumlisha mtoto wangu,” anasema Yevheniya.

Katika miezi ya kwanza ya vita, familia hii iliishi na marafiki zao, walikuwa walivumilia milio ya ving’ora vingi vya mashambulizi ya anga na hata kurushwa makombora. Kila king’ora kilipolia, Yevheniya alimfunika mwanaye kwenye blanketi na kukimbilia chumba cha chini. Huko pia, maziwa ya mama yalimwokoa.
“Nikiwa nimemshika mikononi mwangu wakati wa kurushwa makombora, sikuzote nilikuwa na hofu na kufikiria ni nini kingeweza kumpata. Wazo pekee lililonifanya nifurahi ni kwamba angalau nilipata fursa ya kumlisha.”

Kuna wakati maziwa yake yalipungua ghafla kutokana na kuumwa, kukosa usingizi, joto la hali ya juu na msongo wa mawazo, Yevheniya alianza kusoma makablasha kuhusu unyonyeshaji yaliyochapishwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia watoto UNICEF.
“Nilikuwa nikifuata mapendekezo yaliyolenga kusaidia katika hali kama hizo, kama vile kumshika mtoto karibu na titi langu na kuweka maji," anasema. "Pia nilikuwa nikijaribu kutuliza hali yangu ya kihemko."
Tangu mwezi Machi 2022, UNICEF imekuwa ikifanya kampeni za kutoa habari kusaidia unyonyeshaji nchini Ukraine. Zaidi ya akina mama milioni 1 tayari wamepokea taarifa kuhusu maandalizi sahihi na mambo mbalimbali wanayopaswa kurekebisha ili waweze kuendelea kunyonyesha.