
Tangu angali mdogo, Phayvieng Vongkhamheng alikuwa na hisia kwamba maisha ya kijijini na nyikani yalichanganyikana kimaisha.
"Mara ya kwanza nilipoenda msituni karibu na kijiji changu, nilikuwa na umri wa miaka 10. Nilipenda msitu kwa sababu niliweza kukusanya njugu, uyoga, vyura, na samaki nikiwa na baba yangu. Miti ilikuwa mizuri sana msituni na ilikuwa mirefu sana.”

Hali hiyo ya kupenda misitu na mazingira iliendelea kukaa kichwani mwa Vongkhamheng, wakati wa uharibifu (ukataji miti, uvamizi wa maeneo ya pori, ujangili), na vile vile wakati wa neema ya mavuno. Matokeo yake sasa amekuwa sehemu muhimu katika mafanikio ya mazingira ya eneo lake.

Hali iliendelea kuwa nzuri na yakupendeza na kuenea kote nchini Lao.
Lakini huko Thailand na Cambodia, idadi ya Kulungu pamoja na maeneo mengine ya dunia walikuwa hatarini kutoweka na walipungua kwa zaidi ya asilimia 50. Katika kipindi cha miaka 15 iliyopita idadi ilishuka na kufikia takriban Kulungu 1,500 tu ambao ndio waliosalia porini.
Lakini huko Laos, Bw. Vongkhamheng ana hadithi tofauti ya kusimulia.

Bw. Vongkhamheng ni Meneja Msaidizi wa Mradi wa ‘Usimamizi Endelevu wa Misitu na Ardhi Kusini mwa Lao.
Mradi huu unatekelezwa na Idara ya Misitu, kwa ufadhili wa Global Environment Facility (GEF) na msaada wa Shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa maendeleo duniani, UNDP, mradi huo umekuwa ukikuza usimamizi endelevu wa ardhi na misitu katika mifumo ikolojia ya misitu na ulinzi wa makazi muhimu ya wanyamapori na bayoanuwai yake.

Mradi huo wa Mfumo wa Ikolojia SALAMA au SAFE umewezesha mabadiliko ya kuelekea usimamizi endelevu wa ardhi na misitu katika mandhari ya misitu ya Mkoa wa Savannakhet.
Matokeo yamekuwa makubwa: Iidadi ya kulungu walio hatarini kutoweka imeongezeka zaidi ya mara mbili, kutoka 80 mwanzoni mwa mradi hadi zaidi ya 170 hivi sasa.

Mafanikio haya (ingawa bado ni tete) yanachagizwa kwa sehemu na ushirikiano mzuri wa jamii. Ushirikishwaji wa jamii umejumuisha upangaji wa matumizi ya ardhi, mikataba ya uhifadhi, doria za walinzi, elimu ya mazingira na kuongeza uelewa, pamoja na usaidizi wa maisha endelevu.