
Nchi ya Malaysia ina mifumo ya mito 157 pamoja na aina mbalimbali za ardhioevu ya kitropiki, misitu, na mifumo ya ikolojia ya baharini, inayowakilisha zaidi ya maeneo 200 ulimwenguni.
Kutokana na mifumo hiii nchi hii inatambulika kama mojawapo ya nchi 17 zenye utofauti mkubwa duniani kwakuwa mifumo yake ya mito na misitu inaunga mkono utofauti mkubwa wa viumbe hai wa majini na nchi kavu.
Mifumo hii ya ikolojia inajumuisha zaidi ya aina 600 za samaki wa majini, wote wameunganishwa katika mtandao wa ulinzi wa huduma za mfumo ikolojia, kutoka kwenye maji safi na uzalishaji wa chakula hadi kudhibiti mmomonyoko wa udongo na kuzuia mafuriko.

Eneo la juu la Bonde la Mto Kinta (Perak) linazunguka eneo la takriban hekta 18,000 katikajiji la Ipoh huko Perak. Mradi huu umejikita katika usimamizi wa eneo la juu la Sg Kinta ambalo ni muhimu kwa uhifadhi wa bioanuwai na kuhakikisha kuna usambazaji wa maji.
Katika mpango wa majaribio ya mradi huo kupitia utumiaji wa suluhu za asili, mradi umekuwa ukitumia mbinu za uhandisi wa kibaolojia ili kupunguza mmomonyoko wa udongo na hatimaye kuzuia mchanga kuteremka chini ya mkondo, na pia kuboresha maisha ya jamii za kiasili katika eneo hilo.

Kazi hii imehusisha kuwashirikisha wadau wa maeneo hayo ikiwa ni msisitizo wa kushirikishana na kuziwezesha jamii asilia za eneo la Orang Asli.
Pamoja na kuboresha kikamilifu uelewa wa wananchi kuhusu mazingira na ufuatiliaji wa uchafuzi wa mito, wanajamii wa eneo la Orang Asli walifundishwa na kuajiriwa katika kazi ya uhandisi wa kibaiolojia ili kusaidia kupunguza na kudhibiti mmomonyoko wa mteremko katika sehemu iliyochaguliwa ya vyanzo vya juu vya maji.

Zaidi ya warsha za kiufundi na za kujenga uwezo, maeneo manne ya uhandisi wa viumbe yalianzishwa, na kitalu cha mianzi na mimea mingine muhimu kwa ajili ya kukabiliana na mmomonyoko wa udongo kilianzishwa katika Kijiji cha Orang Asli Kampung Pawong.

Kwa mara ya kwanza kabisa, katika kikao cha Tano cha Baraza la Mazingira la Umoja wa Mataifa (UNEA5) ulimwengu ulikubaliana juu ya ufafanuzi rasmi wa suluhu zinazotegemea asili.
Azimio hili la msingi liliweka wazi kwamba ili kufikia Malengo ya Maendeleo Endelevu SDGs ni wakati wa kuimarishwa kwa hatua za kulinda na kurejesha asili.
Mradi huu wa UNDP wa Malaysia unaonesha thamani ya uhandisi na asili.