
Kamanda kikosi TANZBATT 7 Luteni Kanali John Ndunguru ( wa kwanza kulia) akiangalia ramani kwa makini wakati wa ukaguzi wa barabara inayotoka kijiji cha Mbau kuelekea Kamango ambapo barabara hiyo ilikarabatiwa kwa msaada wa MONUSCO kupitia kikundi chake cha uhandisi cha Indonesia huku TANZBATT 7 ikitoa ulinzi kwa kikundi hicho dhidi ya waasi wa ADF.

Kamanda kikosi cha TANZBATT 7, Luteni Kanali John Ndunguru (wa pili kushoto) akizungumza na mmoja wa maafisa wa jeshi la DRC, FARDC (wa kwanza kushoto) ikiwa ni sehemu ya ushirikiano na Tanzabatt katika kuhakikisha usalama wa vikosi hivyo vya MONUSCO.

Kamanda wa kikosi cha Tanzania kwenye ujumbe wa MONUSCO, Luteni Kanali John Ndunguru akizungumza na Ostech Mputi (katikati) ambaye ni mkalimani wa lugha za kikongo na kifaransa. Bwana Mputi ameajiriwa na MONUSCO kusaidia kuleta maelewano kati ya walinda amani na wenyeji kupitia matumizi ya lugha ya wenyeji DRC.