Wanawake hawa wawili wa kiswidi ni askari wa majini ambao walikuwa sehemu ya timu ya ushiriki wa jamii na walinda amani katika operesheni ya Umoja wa Mataifa nchini Mali (MINUSMA) mnamo 2018. Uswidi ni kati ya nchi zinazo ongoza kuchangia kwa kutoa wanawake walinda amani wa Umoja wa Mataifa
Msaada wa kimatibabu kwa jamii za mitaani ni moja kati ya njia nyingi ambazo walinda amani wa Umoja wa Mataifa wanatumia ili kusaidia kuimarisha maisha ya raia na kusaidia kujenga na kuimarisha uaminifu.
Hapa, wahudumu wa afya wa kijeshi wa Afrika Kusini katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo wanatoa msaada wa kwanza kwa mtoto.
Huko Liberia, polisi wanawake wanahudumu kutoka Kitengo cha Polisi raia wa China kilichopelekwa kwa operesheni ya kulinda amani ya ya Umoja wa Mataifa UNIL.
Walishiriki katika doria wakasaidia katika kutoa ushauri kwa maafisa wa polisi wa Liberia na kufanya kwa upana na kwa kina shughuli za kufikia na kuelimisha jamii za mitaa.
Kitengo cha polisi cha Bangladeshi kilifika Haiti mnamo 2010 kufanya kazi na walinda amani wa Umoja wa Mataifa nchini humo.
MINUSTAH. Bangladesh ni kati ya nchi chache ambazo zimetoa msaada wa kuchangia wanawake walinda amani karibia wote katika kulinda amani ya Umoja wa Mataifa.
Wanawake walinda amani wamehusika pia katika mapambano dhidi ya ugonjwa huo wa COVID-19, kusaidia viongozi wa kitaifa na kusaidia kulinda jamii zilizo hatarini.
Hapa, afisa wa polisi wa Indonesia katika Jamhuri ya Afrika ya Kati anaonyesha wavulana huko Bangui jinsi ya kunawa mikono yao ili kuzuia kuenea kwa virusi.
Raia wana jukumu muhimu katika operesheni za kulinda amani za Umoja wa Mataifa kote ulimwenguni. Huko Mali, afisa wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa (katikati) anahojiana na shuhuda katika mji wa Menaka kama sehemu ya uchunguzi wa mauaji ya watu kadhaa na washambuliaji wenye silaha.
Na huko Sudani Kusini, waandishi wa habari wanaofanya kazi katika redio ya Umoja wa Mataifa ya Miradi ya Miraya inachangia kujenga amani, kwa kuleta jamii pamoja kujadili changamoto zao lakini pia matarajio yao ya pamoja.
Leo, vituo vya redio vya kulinda amani katika nchi nyingi, kama vile Mali, Jamhuri ya Afrika ya Kati na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo,DRC hivi sasa vinatoa habari muhimu wakati wa janga la COVID-19.
Wanawake zaidi katika utunzaji wa amani inamaanisha usalama bora wa kulinda amani, na shughuli bora na utendaji.
Kikosi cha Kulinda amani cha Umoja wa Mataifa nchini Cyprus (UNFICYP) ilikuwa dhamira ya kwanza kuwa na wanawake wakati huo huo wakiongoza raia wake, jeshi na polisi.
Hapa, Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu huko Cyprus na Mkuu wa UNFICYP, Elizabeth Spehar, na Kamanda wa Jeshi Mkuu Meja Jenerali Cheryl Pearce, anakukagua ramani za maeneo walinda amani wanakotumwa kufanya kazi.