
Wakati wa kukusanya chakula watu wamegawanywa katika vikundi vidogo na huulizwa kukaa mbali mbali mita 1.5 kando ya mwingine. Vituo vya kuosha mikono vimewekwa katika tovuti za usambazaji wa chakula, na vifaa vya kinga ya kibinafsi kupewa wafanyakazi. Jamii hupokea muhtasari wa kina na kwa kina juu ya ugonjwa wa COVID-19 na hatua za kuuzuia.

Katika kambi za wakimbizi za Kakuma na Dadaab nchini Kenya, WFP hutoa chakula kwa watu zaidi ya 400,000 kila mwezi. Picha iliyomo hapa inaonyesha mfanyakazi wa misaada za kibinadamu katika mavazi ya kinga akithibitisha kitambulisho cha mkimbizi anayepokea msaada wa chakula huko Kakuma, kwa kutumia skna ya kibodi anaonyesha utumizi wa alama za vidole na alama za iris ambazo kwa sasa zimesimamishwa kwa sababu ya hatari ya kuenea kwa maambukizi wa Corona.

Nchini Zimbabwe WFP inaanda hatua za kudhibiti hatari zozote zitakazozuka katika mgao wa chakula ili kukabiliana na janga la COVID-19. Imeongeza idadi ya sehemu za kufanyia mgawanyo ili kuzuia watu kuzidi na kujazana kupita kiasi, kusambaza mavazi ya kujikinga na vifaa vya afya na usalama kwenye uwanja, Shirika hili limeweka vifaa vya kuosha mikono, na kuhakikisha kwamba watu hawatangamani. WFP na washirika wake wamezindua kampeni ya mawasiliano kupitisha habari muhimu za kiafya na njia za kujikinga, kupitia kutuma jumbe vupi kwenye simu za mkono, redio na mikutano ya watu wachache.
Picha hapa chini zote zilichukuliwa kwenye usambazaji wa chakula wilayani Shamvu.

Kutochangamana sasa ni jambo la kawaida katika ugawaji wote wa chakula nchini Zimbabwe. Watu hujipanga katika vikundi vya watu watano, waliowekwa nafasi kubwa kati yao, ilikukusanya chakula chao cha kila mwezi cha unga wa mahindi, mgawanyiko wa mbaazi na mafuta ya mboga. Chakula hiki ndio tumaini la maisha kwa mamilioni ya raia wa Zimbabwe hivi sasa kwenye kilele cha msimu wa njaa.

Wataalam wa teknolojia wa Shirika la mpango wa chakula la Umoja wa Mataifa wamesambaza vifaa vya kushika kwa mkono kwa maeneo yote ya wafanyikazi walio nje ya ofisi ili waweza kutumia kadi ya SCOPE kwa mbali bila kushika kwa mkono wao, na pia watu wanaweza kuthibitishwa kwa njia isiyo na kugusana.
Gloria Kamudemeta, mfanyakazi wa afya wa kijijini kutoka Serikali ya Zimbabwe, alisema: "Tupo katika mgao wote wa chakula wa Shirika la mpango wa chakula la Umoja wa Mataifa. Tukielimisha watu na kutoa mafunzo kuhusu kuenea kwa virusi hivi. Tunahakikisha kila mtu anaosha mikono yao, ilituweze kudhibiti virusi hivi la sivyo Zimbabwe haitasonga mbele.

Rebecca Kapaira, mama wa watoto watano nchini Zimbabwe, akipokea chakula tofauti pamoja na mafuta ya mboga, katika kijiji cha Madziwa, wilaya ya Shamva, Zimbabwe anasema, "nimefurahia kuwa WFP iliendelea kuleta chakula mwezi huu, licha ya kuwa mambo hayaendi kama kawaida nchini kutokana na janga hili la corona. Ukosefu wa chakula inamaanisha njaa zaidi kwa familia zetu. Kuangalia kile nilichopanda kwenye shamba langu, hakukuwa na chochote cha kuvuna, kwa hivyo ikiwa sio kwa WFP, sijui ningefanya nini kwa watoto wangu. "