Bwana Pérez de Cuéllar alisimamia uanzishwaji wa kungi la mpito la Umoja wa Mataifa la usaidizi nchini Namibia, UNTAG, ambalo lilisaidia mchakato wa uhuru na kisha kufanyika kwa uchaguzi huru na wa haki. Pichani akikagua kikosi cha wanajeshi kutoka Kenya kwenye mji mkuu wa Namibia, Windhoek, hii ilikuwa mwezi Julai mwaka 1989.
Bwana Pérez de Cuéllar alianza harakati za kidiplomasia nchini Peru mwaka 1940 na pia alikuwa Waziri Mkuu wa taifa hilo la Amerika ya Kusini. Mwezi Oktoba mwaka 1985, akiwa Katibu Mkuu wa UN alimkaribisha kwenye makao makuu ya umoja huo jijini New York, Marekani, Mama Teresa, kiongozi wa shirika la watawa wa kujitolea.
Mwelekeo wa dunia ulibadilika kwa kiasi kikubwa na haraka wakati Bwana Pérez de Cuéllar akiwa Katibu Mkuu wa UN. Kuanzia vita vya baridi kati ya Marekani na Urusi. Mwaka 1988, alikutana na Rais Mikhail Gprbachev wa uliokuwa Muunganowa Kisovieti ambapo katika mazungumzo hayo Bwana Gorbachev alimkabidhi Bwana Pérez de Cuéllar zawadi ya Umoja wa Mataifa.