
Mamia ya maelfu ya watu katika ziwa Chad liliko barani Afrika wamelazimika kuhama kwa sababu ya ukosefu wa usalama uliosababishwa na vikundi vya waasi vilivyojihami. Wengi, waliotekwa nyara na kuteswa mikononi wa vikundi hivyo hivi sasa wanaishi katika kambi za wakimbizi na makazi yaliyoko huko Cameroon. Wala Matari anatoka Cameroon na mmoja wa mamia ya maelfu ya watu waliokimbia nyumba zao katika eneo la ziwa Chad kufuatia shambulio la waasi wao waliojihami. "Walikuja usiku wa manene, wakati nilikuwa nimelala na watoto wangu."

Alitekwa nyara na kuvushwa mpaka hadi nchini Nigeria ambapo aliishi miaka miwili msituni. "Watu wengine walijaribu kutoroka lakini walikamatwa na walikufa kutokana na majeraha yao. Masikio, matiti au miguu yao ilikatwa na waliachwa wafe msituni.”

Aliokolewa na "wanaume waliovalia sare za kijeshi" na sasa anaishi kwenye Zamai huko Cameroon, pamoja na watu wengine waliokimbia makwao kutokana na ugaidi. "Ninaenda kanisani kuondoa huzuni yangu, kuondokana na kumbukumbu mbaya. Tunalala salama zaidi baada ya kusikia neno la Mungu. Baada ya misa nashukuru kuwa niko hai. ”

Mohammed Lawan Goni anaishi kambi ya wakimbizi ya Minawao iliyoko nchini Cameroon. Kambi hii inayohifadih wanigeria iko kilomita nane kutoka makazi ya Zamai Yeye zamani alikuwa ni afisa mtoza kodi wa serikali na alikimbia Nigeria baada ya magaidi kushambulia mji wa ulioko Banki.

“Nilitekwa na vijana wawili barubaru kutoka katika mji wangu. Nilikuwa nazifahamu familia zao na walitaka kukata shingo yangu.”
Wapiganaji wawili watu wazima waliingilia kati na hivyo akapona. “Kama wakitubu, nitawasamehe. Lakini ni Allah atakayetuhukumu.”

Mohamed Lawan Goni ameishi katika kambi ya Minawao na wake zake wawili, watoto 10 na mama yake kwa takribani miaka mitano. “Kwanza, tunahitaji amani, ili kwenda na kuona hali ya nyumba zetu, Mashamba yetu ambavyo viliteketezwa kwa moto. Kama wakituambia hali imetengamaa huko Nigeria, tutaenda. Kama sivyo, tutabaki hapa hadi kifo chetu kitakapokuja.”

Fati Yahaya kutoka Nigeria, yeye pia anaishi katika kambi ya Minawao. Aliishi miaka mitatu na magaidi wapiganaji huko kaskazini mwa Nigeria. “Nilipigwa mara nyingi kama ningeshindwa kufuata maelekezo yao, kwa mfano, kutowaangalia wanaume usoni. Baadhi ya watu walipigwa hadi kufa, wengine walifariki kwa njaa. Niliishi kwa hofu kuwa mimi pia nitauawa.”