Wanawake wa Sweden wachukua jukumu gumu la ulinzi wa amani UN


Mwaka 2018 wanawake 25 walipelekwa Mali kwenye kikosi kilichokuwa na wanajeshi 252 kutoka Sweden. Hapa ni mwanamke mlinda amani wa Kiswidish akiwa katika doria mjini Timbuktu Kaskazini mwa taifa hilo la afrika Magharibi.UN Photo/Harandane Dicko

Mali ni moja ya eneo la operesheni za ulinzi wa amani za Umoja wa Mataifa zenye changamoto kubwa. Wahudumu na walinda amani kutoka Sweden wamekuwa wakipelekwa Mali tangu mwaka 2014.UN/Harandane Dicko

Sweden ilianza kuchangia vikosi kwenye operesheni za ulinzi wa amani za Umoja wa Mataifa mwaka 1948 na tangu wakati huo zaidi ya wanawake na wanaume 80,000 kutoka Sweeden wameshiriki operesheni mbalimbali za ulinzi wa mani za Umoja wa Mataifa ikiwemo kwenye kikosi cha dharura cha Umoja wa Mataifa nchini Misri (UNEF) mwaka 1956 kama wanavyoonekana pichani. UN Photo/GJ

Kufuatia kuanzishwa jeshi la kulinda amani la Umoja wa Mataifa nchini Cyprus (UNFICYP) mwaka 1964, Sweden ilipeleka kikosi kwenye kisiwa hicho kilichoko kwenye bahari ya Mediterranea. UN Photo

Wanawake siku zote wamekuwa na mchango na jukumu muhimu katika operesheni za ulinzi wa amani za Umoja wa Mataifa. Wanawake 12 kutoka kikosi cha askari watembea kwa miguu walikuwa wanawake wa kwanza walinda amani kujiunga na mpango wa Umoja wa Mataifa nchini Cyprus, UNFICYP, 1979. UN Photo/John Isaac

Nchini Sudan Kusini, Sweden imepeleka maafisa wa polisi ambao ni sehemu ya mpango wa Umoja wa Mataifa nchini humo UNMISS. Hawa ni baadhi ya maafisa hao wa polisi wa wakichangamana na wakimbizi wa ndani katika moja ya makazi ya ulinzi wa Rais ya Umoja wa Mataifa mjini Juba.UNMISS/Nektarios Markogiannis

Nchini Timor Leste, mwaka 2010, maafisa wa polisi kutoka Sweden wakiwa sehemu ya mpango wa Umoja wa Mataifa nchini humo, UNMIT. Hapa afisa kutoka Sweden akiwa pamoja na mwenzake wa kutoka China wakiwa kwenye kituo cha kulea watoto yatima kwenye mji mkuu Dili.