
Vikosi vya kwanza vya Ghana vilivyotumwa kama sehemu ya operesheni ya walinda amani wa Umoja wa Mataifa kusaidia kurejesha utulivu nchini Jamhuri ya ya Congo ya zamani (ONUC). Pichani ni polisi wa Ghana mwezi August mwaka 1960 wakiwa mjini Leopoldville ambayo ni Kinshasa ya sasa. UN /HP

(Yasser Arafat katikati), Mwenyekiti wa Kamati kuu ya chama cha ukombozi wa Palestina (PLO) akizungumza na wanahabari mjini Beirut kufuatia kukubali kwake wito wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kusitisha mapigano kusini mwa Lebanon mwezi Machi mwaka 1978. Miongoni mwa waliosimama pamoja naye ni Meja Jenerali Emmanuel Erskine wa Ghana (wa pili kutoka kushoto), kamanda wa mpito wa vikosi vya mpito vya Umoja wa Mataifa nchini Lebanon (UNIFIL). UN /John Isaac

Askari wa Ghana (anayezungumza katika redio) na askari kutoka China wakiwa katika eneo lisilokaliwa na majeshi katika mpaka wa Iraq na Kuwait mwezi Mei mwaka 1991. Eneo hilo lilikuwa kilomita 10 kuingia Iraq na kilomita 5 kuingia Kuwait kutokea katika mipaka kama ilivyokubaliwa mnamo mwaka 1963.UN /John Isaac

Maafisa wa jeshi la Umoja wa Mataifa waliokuwa wakihudumu na mamlaka ya mpito ya Umoja wa Mataifa nchini Cambodia UNTAC, wakielekeza vyombo vya usafiri katika mji mkuu Phnom Penh, mwezi Januari mwaka 1993. Kulia ni ni afisa wa polisi kutoka India, wa pili ni afisa wa polisi kutoka Ghana.UN/Pernaca Sudhakaran

Askari wa vikosi vya pamoja vya kulinda amani Darfur kutoka Muungano wa Afrika AU na Umoja wa Mataifa, UNAMID, wanaotoka Ghana, Indonesia na Nigeria wakiwa katika doria za kila siku kuangalia hali ya usalama katika kambi ya wakimbizi wa ndani ya Zam Zam mwezi April mwaka 2009. UN Photo/Olivier Chassot

Akisaidiwa na wenzake wawili, Angela Ama Agyeman Sesime (katikati) wa Ghana, Polisi mshauri wa UNAMID akiandika ripoti baada ya doria katika kambi ya Zam Zam ya kuwahifadhi wakimbizi wa ndani eneo la Darfur Kaskazini, Sudan, Oktoba 2010. UN/Olivier Chassot

Mmoja wa wahandisi wa Ghana wanaohudumu katika ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kuweka utulivu nchini Mali, MINUSMA nchini Mali, akipaka rangi ukuta wa shule iliyoko Taliko, kwenye makazi duni katika viunga vya mji mkuu Bamako. Kazi hiyo ilikuwa ni sehemu ya juhudi mwishoni mwaka 2013 kuboresha shule ambayo ilikuwa imezipokea familia zilizokuwa zimepoteza makazi kutokana na mafuriko mapema mwaka huo. UN/Marco Dormino

Tangu mwezi April 2017, kikosi cha askari kutoka Ghana wanaohudumu katika mpango wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini UNMISS wamekuwa wakitoa huduma inayohitajika sana ya tiba kwa wanyama kwa ajili ya watu wanaowazunguka na kote Bentiu. Huduma hizo ni sehemu ya juhudi zao za kujenga amani ya kudumu na kuwasaidia watu wa Sudan. UNMISS/Nektarios Markogiannis

Kikosi cha Ghana kinachohudumu katika ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Lebanon UNIFIL wanaonekana wakitoa huduma ya matibabu katika Al Kawzah, Lebanon Kusini mwezi Januari 2016. Ghana ni moja ya wachangiaji wakubwa wa vikosi katika UNIFIL wakifanya shughuli kama vile doria, uangalizi wa eneo kubwa la kilomita 120 la mstari wa Buluu linalotenganisha Lebanon na Israel na pia wakiratibu msaada wa kibinadamu.UN/Pasqual Gorriz