
Huduma za walinda amani wanaume na wanawake wa Nepal hazijakuja bila kulipa gharama, walinda amani 76 kati yao wamepoteza maisha wakihudumu chini ya bendera ya Umoja wa Mataifa katika kipindi cha miongo sita iliyopita. Walinda amani wa Nepal wanaofanya kazi katika operesheni za Umoja wa Mataifa nchini Burundi wanaonekana hapa wakiwasili katika mji wa Isale ili kuangalia masuala ya usalama na wakazi wa eneo hilo Desemba 2004. Picha na UN / Martine Perret

Wajumbe wa kikosi cha walinda amani wa Nepali wakiwa katika doria ya ulinzi-wa-raia huko Juba mwezi Mei 2015. Vikosi vya Nepal husaidia kuwalinda raia nchini Sudan Kusini kwa kushika doria na kuwezesha usafirshaji wa misaada ya kibinadamu nchini humo na kutoa mazingira salama kwa wakimbizi wa ndani wanaoishi katika kambi za ulinzi wa raia za Umoja wa Mataifa.

Walinda amani kutoka Nepal kwa sasa wanahudumu katika operesheni 14 kote ulimwenguni, ikiwa ni pamoja na maeneo hatari kiusalama kama Mali, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) na Jamhuri ya Afrika ya Kati (CAR). Pichani ni wanaume kwa wanawake wa kitengo cha Polisi cha Nepal walioko katika ujumbe wa Umoja wa Mataifa huko CAR (MINUSCA) wakati wa hafla ya opokeaji medali mwezi Machi 2018. Picha ya UN / Dany Balepe

Kikosi maalum cha walinda amani wa Nepal wanaohudumu katika kikosi cha pamoja cha Umoja wa Mataifa na Muungano wa Afrika Darfur Sudan (UNAMID) wakiwa katika kampeni za kutoa huduma za afya katika kijiji cha Kuma Garadayat mwezi Mei 2011. Tukio hilo lilikuwa ni jitihada za kufikisha misaada katika maeneo ambayo yalikuwa vigumu kuyafikia kwa muda mrefu kutokana na vita Picha na UN / Albert Gonzalez Farran.

Walinda amani kutoka Nepal wanaofanya kazi na ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Mali (MINUSMA) wanafanya zoezi la uteguzi wa mabomu ya ardhini katika uwanja wa ndege wa Kidal Septemba 2015 kabla ya ziara ya Kamanda wa Jeshi la Ujumbe huo . Picha na UN / Marco Dormino