
Alice wakati akishiriki harakati za ujenzi wa soko la Mutambara nchini Burundi. Shirika la mpango wa maendeleo la Umoja wa Mataifa, UNDP nchini Burundi kupitia mradi wa ujenzi wa kushirikisha jamii, waliweza kujumuisha wananchi kwenye kazi za ujenzi wa soko na hatimaye kuwapatia kipato cha kunusuru kaya zao.

Hapa ni kwenye shamba la samaki la Daukandi nchini Bangladesh, wavuvi wakivuna mazao yao baada ya kufuga samaki kwa kuzingatia mbinu bora za ufugaji wa samaki kutoka shirika la chakula na kilimo, FAO. Uvuvi bora unasaidia kuongeza kipato cha wakulima na wafugaji.

Kwenye mji wa Gao, nchini Mali, kijana akiwa kwenye banda la kuku ambao anafuga kufuatia msaada kutoka ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kuweka utulivu nchini Mali, MINUSMA. Ujumbe huu kupitia miradi yake ya matokeo ya haraka inasaidia jamii kujikwamua kiuchumi kwa njia ya miradi ya kilimo na ufugaji.

Mkulima kwenye eneo la Gao nchini Mali akionyesha mavuno ya bamia kutoka kwenye shamba ambalo mafanikio yake ni matokeo ya mradi wa ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kuweka utulivu nchini Mali, MINUSMA. Mradi huo wa matokeo ya haraka umesaidia kwenye eneo hilo lililogubikwa na ghasia.

Wanawake wakimbizi wa ndani kwenye kitongoji cha Kati, mkoa wa Koulikoro nchini Mali wakionyesha nguo ambao wametia rangi, kutokana na mradi wa matokeo ya haraka wa ujumbe wa Umoja wa Mataifa aw kuweka utulivu nchini Mali, MINUSMA. Mradi huu unawezesha wanawake kama hawa kuuza nguo hizo waliozoongezea thamani na kupata kipato.

Sasa imekamilika. Batiki hii iko tayari kuuzwa na ni kazi ya mikono ya wanawake wakimbizi wa ndani kutoka kitongoji cha Kati, mkoa wa Koulikoro nchini Mali. Kazi hii in matokeo ya mradi wa matokeo ya haraka wa ujumbe wa Umoja wa Mataifa aw kuweka utulivu nchini Mali, MINUSMA. Mradi huu unawezesha wanawake kama hawa kuuza nguo hizo waliozoongezea thamani na kupata kipato.

Zaidi ya wanufaika 100 wa miradi ya matokeo ya haraka, QIP nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, CAR wameanza kuona matunda ya miradi huio huko Birao, eneo la kaskaizni-mashariki mwa nchi hiyo. Miongoni mwa miradi hiyo ni bustani za mboga na pamoja na kuongeza kipato, mradi umeleta pamoja jamii hiyo ambayo kwa muda imegubikwa na mzozo.