Makundi ya asasi za kiraia yapo ili kuwakumbusha wafanya maamumuzi mara kwa mara kwamba muda unayoyoma wa kuchukua hatua dhidi ya mabadiliko ya tabianchi.wakati mwaka huu tamko la haki za binadamu likitimiza miaka 70 kwamba hatua za mabadiliko ya tabianchi zinatakiwa kwenda sanjari na utekelezaji wa haki za binadamu
Likiwa limetembea kwa mguu kutoka Vatican hadi Katowice “kundi la mahujaji wa hali ya hewa” limewasilisha ujumbe wa haraka na muhimu kwa mkuu wa ofisi ya ya Umoja wa Mataifa ya mabadiliko ya tabianchi, Patrcia Espinosa(kushoto). Miongoni mwao ni Joanna Sustento, ambaye alipoteza karibu kila kitu wakati wa kimbunga Haiyan kilipopiga Ufilipino mwaka wa 2013.
Jukwaani ni mcheza filamu wa zamani na aliyewahi kuwa Gavana wa jimbo la California Marekani, Anold Schwartzenegger pamoja na mkuu wa mkutano wa UN kuhusu mabadiliko ya tabianchi , Patricia Espinosa, mwakilishi wa jamii ya watu asili wa Sahel Hindou Ibrahimna rais wa COP24 Michal Kurtyka, viongozi wa kisiasa, wawakilishi wa asasi za kiraia na maafisa wa Umoja wa Mataifa wakiungana kuhakikisha kazi ya kuchukua hatua dhidimabadiliko ya tabianchi inakamilika.
Hatua dhidi ya madadiliko ya tabianchi ni kuhusu kuinusuru dunia kwa ajili ya kizazi kijacho, watoto na vijana walialikwa jukwaani.
Greta Thunberg, mwenye umri wa miaka 15, ambaye ni mwanaharakati kutoka Sweden alikuja kusema, “ Asilani si wadogo wa kuleta kuweza kuleta mabadiliko.”
Katika mabanda mbalimbali nchi na mashirika tofauti wameonyesha miradi ya kutuweka katika njia ya kupunguza ongezeko la joto duniani hadi nyuzi joto 1.5. kuanzia mitambo mipya ya kisasa inayotumia upepo, magari ya umeme juhudi za upandaji miti pia ngano ambayo inaweza kumea katika eneo bapa la ardhi