Mchakato wa kupata nyaraka rasmi za Umoja wa Mataifa mwaka 1948


Kikao cha Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kikiendelea, wajumbe wakisikiliza kwa makini hotuba. Kisichoonekana ni wahusika wa kunakili kikao hicho kwa njia ambazo zinahakikisha kinachowekwa kwenye kumbukumbu ni kile kilichojadiliwa na si vinginevyo.

Waandishi wa hati mkato walitegemewa sana wakati huo. Hata hivyo binadamu ni binadamu, anaweza akakosa neno moja na hivyo kuharibu mwenendo mzima. Ili kuepusha hali hiyo, mashine kama hiyo pichani ilitumika kunasa sauti ili kuhakikisha kilichoandikwa ni sawa na kilichorekodiwa na mashine .

Wajumbe huwa wana saa 48 kuhakiki hotuba zao na pia kuweza kutuma masahihisho kwa wahariri ili yaweze kuyajumuishwa katika nakala iliofanyiwa marekebisho. Kazi hiyo ni ngumu kama vile kukagua herufi na maandishi kuwa ni sawa na huweza kuandikwa kwenye ubao ili kuona kwamba kuna uwiano.

Nyaraka baada ya kuhakikiwa kuwa iko sawa, kazi inayofuatia ni kutafsiri kwa lugha nyingine. Pichani katibu muhtasi akichapa nakala huku mwingine akitafsiri.

Muswada wa kikao umeshakamilika na uko tayari kwa ajili ya kuchapishwa na kutolewa nakala nyingi. Pichani wapiga chapa wakiwa kwenye hatua za mwisho.

Nyaraka tayari zimekamilika, na pichani ni nyaraka rasmi za Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa. Iliyofunguliwa iko katika lugha ya kirusi, ilihali nyaraka zingine ni katika lugha nyingine rasmi za Umoja wa Mataifa ambazo ni Kiingereza, Kifaransa, Kichina na Kispanyola.