Kijiji cha kwanza kinachotumia teknolojia inayojali mazingira kilifunguliwa mwaka 2011 na Rais wa Rwanda Paul Kagame. Mchakato wa kuanzisha kijiji hicho ulishirikisha wanawake na wanaume. Kijiji hicho kipya kilikuwa mfano. Mfumo huu ulijumisha mipango kadhaa ya ulinzi wa mazingira na kijamii ambazo zilisaidia watu kukuza vipato vyao, kuboresha lishe, kuimarisha usalama wa chakula, kulinda rasilimali za kiasili, kusomesha watoto, na kujenga nyumba zenye viwango vya juu kwenye nchi ambayo licha ya maendeleo, watoto wanne kati ya kumi bado wana utapia mlo, asilimia 40 ya watu bado huishi katika hali ya umaskini, huku mabadiliko ya tabianchi kama ukame, mafuriko na mvua zisizo za kawaida zinaendelea kutishia maisha ya watu.
Vipengele vilivyozingatiwa katika vijiji hivyo ni pamoja na udhibiti wa mabwawa ya maji na kuhakikisha kuwa maji yanapatikana mwaka mzima. Hii inatoa faida za kiafya na kiuchumi kwa kaya za vijiji. Uboreshaji wa usafi wa mazingira hupunguza uenezi wa magonjwa ya maji yanayoambatanishwa na uzalishaji finyu wa kibanadamu. Uanzishaji wa mbinu mpya za kilimo kama vile udhibiti wa mmomonyoko wa udongo na kilimo cha misitu kwa ajili ya kuboresha rutuba ya udongo.
Mapipa ya nishati hai huwezesha familia kutumia nishati safi ya kupika chakula. Utumizi wa nishati hai hupunguza matumizi ya mkaa, huzuia ukataji miti hovyo, hutoa mbolea kwa ajili ya kilimo cha mazao, huongeza viwango vya hewa na kupunguza athari mbaya za chembecheme za moshi. Mapipa haya pia huzuia uchafuzi wa maji na uenezi wa magonjwa ya maji.
Katika vijiji vinavyojali mazingira nchini Rwanda, uvunaji wa maji ya mvua na matumizi ya maeneo ya kuhifadhi maji hayo, hutoa fursa ya kudhibiti mafuriko ya maji na pia huwezesha wanakijiji kuwa na maji ya kutumia kipindi kizima cha mwaka. Hii ni manufaa makubwa ya kiuchumi na kiafya kwa wanakijiji.