
Hivi sasa wafanyakazi 191 wasio askari kutoka Kenya wanahudumu katika sehemu mbalimbali duniani chini ya mwamvuli wa Umoja wa Mataifa duniani, ikiwemo kwenye jimbo la Darfur nchini Sudan, Sudan Kusini, Jamhuri ya Kimekrasia ya Congo DRC, Jamhuri ya Afrika ya Kati CAR na Mali. Hadi kufikia mwezi Juni 2018, Wakenya 62 wamepoteza maisha wakihudumu kwa ajili ya amani.
Katika picha hii ya Julai 2009, Vikosi vya Kenya vikihudumu na mpango wa Umoja wa Maytaifa nchini Sudan (UNMIS) wakifanya doria katika eneo Abyei linalogombewa na wote Sudan na Sudan Kusini.

Makao yake makuu yakiwa El Fasher, Kaskazini mwa Darfurmpango huo unasaidia kulinda raia na kuwezesha usafirishaji wa misaada ya kibinadamu.
Baraza la Usalama hivi karibumi limeongeza muda wa UNAMID hadi mwishoni mwa Juni mwaka 2019, na limepunguza idadi ya vikosi vilivyopelekwa katika eneo hilo kwa lengo la kuondoka kabisa hatimaye.

Mpango wa UNMIL ulianzishwa na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa mwaka 2003 baada ya muafaka wa amani kutiwa saini kumaliza vita vya wenyewe kwa wenyewe. Mpango huo ulihitimisha kwa mafanikio makubwa majukumu yake Machi 2018, muda mfupi baada ya kulisaidia taifa hilo kufanya kubadilishama madaraka ya kisiasa kwa amani baada ya kipindi cha miongo saba.

Ruth Kefa, afisa Magereza wa wa mpango wa Umoja wa Mataifa nchini Liberia (UNMIL), akifurahi wa mwanafunzi wa shule ya upili ya JJ Roberts wakati wa tukio la uelimishaji katika mjini mkuu wan chi hiyo Monrovia, mwezi Oktoba 2012. Wakati UNMIL imekamilisha mpango wake kwa mafanikio makubwa Machi 2018, Jamii ya Umoja wa Mataifa bado ipo nchini humo kusaidia kudumisha amani waliyopata kwa kibarua kugumu.