
Kwa kipato cha karibu shilingi 2000 za Kenya sawa na dola 20 kwa mwezi, Esperanza anajimudu yeye mwenyewe na familia yake iishio kambini. "Ninapenda kuwa mwanamitindo bora zaidi, Lakini fedha ninazozipata ni za kukimu mahitaji yangu ya msingi. Ili kupanua biashara yangu, ninahitaji msaada wa kifedha ambao nitaweza kulipa deni baada ya muda.

Wengi wao huendesha biashara ya maduka madogo. Uchunguzi wa hivi karibuni wa Shirika la Wakimbizi la Umoja wa Mataifa (UNHCR) na Shirika la Fedha la Kimataifa (IFC) umebaini kuwa uchumi katika eneo hilo una thamani ya shilingi bilioni 6 sawa na dola milioni 56. Pamoja na biashara zaidi ya 2000 katika kambi ya Kakuma, wakimbizi wana jukumu muhimu katika kukua kwa uchumi na ujenzi wa ushirika na jumuiya kibiashara ya wenyeji.

Baadhi ya wafanyabiashara zinawahudumia moja kwa moja wakazi, ikiwa ni pamoja na duka hili la kinyozi. Mara nyingi wakimbizi huajiri wenyeji kufanya kazi pamoja nao kama vile kununua mifugo, kuni, mkaa, na bidhaa nyingine kutoka kwa kwa wenyeji .

Ni matumaini kwamba utafiti mpya utaanzisha majadiliano juu ya jinsi sekta binafsi inaweza kuchangia kutafuta suluhisho kwa wakimbizi ndani na nje ya Kenya. Kwa mwana mitindo, Esperanza Tabisha, (Pichani na binti yake) ushirikiano huo tayari unafanya kazi. "Nimeshuhudia jinsi uchumi hapa unakua kwa njia ya biashara. Kakuma ni mahali penye na fursa. "

Katika siku ya wakimbizi ya Dunia, ambayo huadhimishwa kila mwaka tarehe 20 Juni yaelezwa kuwa karibu watu milioni 68.5 wamefurushwa kutoka makwao kote duniani. Idadi kubwa zaidi katika rekodi ya UNHCR. Akizungumza nchini Kenya, Kamishna Mkuu wa wakimbizi duniani, Filippo Grandi alisema: "Tunataka kuanzisha mfumo wa muda mrefu zaidi na endelevu ambao unaweza kuwasaidia wakimbizi na jumuiya ya wenyeji”