Disemba 1958: Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa lapitisha azimio kuhusu “Hoja ya matumizi ya amani ya anga la juu” na kutambua maslahi ya pamoja ya kibinadamu ya anga hilo kwa faida ya wote.
Mwaka uliofuatia Kamati ya matumizi ya amani ya anga za juu ilikutana kwa mara ya kwanza (pichani) katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa New York.
Oktoba 1963: Mwanaume na mwanamke wa kwanza kwenda anga za juu. Yuri Gagarin (kulia) na Valentina Tereshkova ( wa pili kushoto) watembelea makao
makuu ya Umoja wa Mataifa. Pichani wanaonekana na Katibu Mkuu U Thant (wa pili kulia) na Rais wa Baraza Kuu Carlos Sosa-Rodriguez (kushoto).
Julai 1969: Bendera ya Umoja wa Mataifa inaambatana na wanaanga wa Marekani Neil Armstrong, Edwin Aldrin Jr na Michael Collins kwenye safari ya mwezini ya Apollo 11.
Pichani ni wataalamu watatu, Armstrong , (wa pili kushoto), Aldrin, (wa tatu kulia) na Collins, (wa pili kulia) wanatembelea makao makuu ya Umoja wa Mataifa, na Katibu Mkuu U Thant (katikati) akiwa na jiwe kutoka mwezini na bendera (Julai 1970) .
Mei 2004: Yang Liwei, mwanaanga wa kwanza wa kichina kusafiri anga za juu anakukutana na Katibu Mkuu Kofi Annan. Wakati wa mkutano huo, Bw. Liwei alimpatia mkuu huyo wa Umoja wa Mataifa bendera ya Umoja wa Mataifa iliyopeperushwa kwenye chombo cha anga za juu cha Shenzhou 5.
Novemba 2016: Umoja wa Mataifa wamteua mwana anga wa zamani wa Marekani, Scott Kelly, ambaye alikaa kituo cha kimataifa cha anga za juu kwa muda wa mwaka mmoja kuwa bingwa wa kuhamasisha manufaa ya anga za juu kwa maendeleo endelevu.
Pichani Bw. Kelly (kushoto) na Simonetta Di Pippo (kulia), Mkurugenzi wa Ofisi ya Umoja wa Mataifa masuala ya anga za juu (UNOOSA).