
Tangu kuanzishwa kwa operesheni za ulinzi wa amani za Umoja wa Mataifa askari kutoka Ethiopia wamekuwa kiungo muhimu sana katika mchakato wa kuendeleza amani katika maeneo mbalimbali duniani.
Mnamo mwaka 1951 Ethiopia ilishirikishwa katika ulinzi wa amani katika vita vya Korea. Na mwaka 1960 walinda amani wa Ethiopia walikuwa miongoni mwa vikosi vilivyoagizwa na Bazara la Usalama kushiriki operesheni ya ulinzi wa amani katika Jamuhuri ya kidemokrasia ya Kongo.

Mnamo februari mwaka 2010, serikali ya Ethiopia ilitoa helikopta ya kivita kwa Muungano wa Afrika, AU, ili kusaidia vikosi vya ulinzi wa amani kwenye ujumbe wa pamoja wa AU na UN huko Darfur UNAMID, kufuatia ombi la Katibu Mkuu kutaka nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa kutoa vifaa vya kijeshi ili kusaidia walinda amani katika sehemu za migogoro.

Ethiopia ni miongoni mwa nchi zinazoongoza kwa kuwa na walinda amani wengi katika operesheni za Umoja wa Mataifa ambapo, ina askari 8,300, na wengi wao wakihudumu katikaujumbe wa pamoja wa Muungano wa Afrika, na Umoja wa Mataifa Darfur, UNAMID, halikadhalika ujumbe wa ulinzi wa amani wa UN huko Abyei UNISFA na Sudan Kusini UNMISS
Pichani ni walinda amani kutoka Ethiopia wakiongea na watoto wawili wa kiume katika eneo la Gereida, Sudan.

Pichani ni walinda amani wawili wanawake ambao ni mafundi gari, Sajini Meseret Adera naKoplo Seblewegel Demesse. Hawa ni miongoni mwa walinda amani 800 kutoka Ethiopiawanaohudumu UNAMID.
Pichani wako kazini wakitengeneza gari la kijeshi katika gereji ya Gereida kusini mwa Darfur.

Pichani ni msafara wa malori ya misaada kutoka shirika la mpango wa chakula duniani WFP yakipeleka mafuta na chakula kwa ajili ya wamibizi wa ndani. Malori hayo yanasindikizwa na walinda amani kutoka Ethiopia na Rwanda na yanatoka El Fasher yakielekea Shagil Tobaya, kaskazini mwa Darfur.
Safari hiyo ni ya umbali wa kilomita 100, ambapo sehemu kubwa ya barabara hiyo inakabiliwa na changamoto za kiusalama na hata miundombinu mibovu

“Wanawake wana haki ya kufanya kazi yoyote ile bila kubaguliwa” hiyo ni kauli ya BrigediaJenerali Zewdu Kiros Gebrekidan, aliyekuwa Naibu Kamanda Mkuu wa kikosi cha walinda amani cha Umoja wa Mataifa katika jimbo la Abyei, UNISFA hadi mwezi Aprili mwaka 2017.
Huyu ni mfano tosha kuwa wanawake wana nafasi kuu katika kutekeleza kazi za Umoja wa Mataifa kutokana na uwezo wao wa kuziunganisha jamii, hususan wanawake na watoto ambao ni waathirika wakuu katika migogoro