Maeneo 13 yaingia kwenye urithi muhimu wa kilimo duniani


Maeneo hayo mapya yanajumuisha aina mbalimbali za uzalishaji wa kilimo ikiwemo , mboga za majani, chumvi, na kilimo cha mpunga, pia uzalishaji wa nyama, chai, wasabi pamoja na matunda. Wakulima mjini Xiajin, China bado wanazalisha maforosadi kwa kutumia mbinu asilia.

kilimo cha maforosadi China mjini Zhejiang Huzhou, wakati mwingine kinafanyika pembezoni mwa mabwawa ya samaki. Naiu mkurugenzi mkuu wa FAO Maria Helena Semedo anasema “maeneo hayo sio sababu ya kumbukumbu ya kale , bali yanatoa suluhu ya sasa na baadaye.”

Mjini Shizuoka nchini Japan, kilimo cha Wasabi kinafanyika katika mtindo wa kizamani wa matuta, kando ya mfereji.. Maria Helena Semedo ameongeza kwamba maeneo hayo yamechaguliwa ili kuonyesha “ubunifu na fursa ikiwa ni pamoja na kupanua wigo wa masoko mapya na biashara kama , uwekaji chapa unaojali mazingira, kilimo cha utalii, na uwezeshaji vijana ili kuongeza thamani ya mazao ya kilimo.

Mashamba ya kilimo pia yameundwa kwa makusudi katika eneo la Chinampas la Mexico City huko nchini Mexico. Yameundwa kulingana na mbinu za jadi zilizotumiwa wakati wa ustaarabu wa Aztec na ambazo zimepitishwa kwa njia ya simulizi kutoka kizazi kimoja cha wakulima hadi kingine.

Huko Barroso Ureno , mfumo wa kilimo cha ufugaji au agro-sylvo-pastoral ambapo miti hupandwa pamoja na mazao ulikuwa kati ya maeneo ya kwanza ya Ulaya kuwa katika orodha ya mifumo maalum ya urithi wa Kilimo muhimu Kote duniani.

Maeneo teule mapya yanajumuisha uzalishaji wa mizabibu ya Malaga mjini Axarquia nchini Hispania, na kufanya jumla ya maeneo yote muhimu kwa kilimo kote duniani kufikia.