Mkuu wa Sekretariat ni Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ambaye huchaguliwa kwa kupigiwa kura kwa kuongoza miaka mitano, na huweza kuchaguliwa kwa kipindi cha pili na hivyo kufanya mwisho wa uongozi kuwa miaka 10. Miongoni mwa majukumu yake ni kuhakikisha amani na usalama wa dunia unaendelea kuimarika na njia ya diplomasia ndio inayopigiwa chepuo zaidi. Pichani Katibu Mkuu wa UN Antonio Guterres akiwa nchini Pakistan ambapo pamoja na mambo mengine amekwenda kuzungumza kuhusu mzozo baina ya Marekani na Iran nchi ambazo zinahasimiana.
Katika kushughulikia masuala mbalimbali ya dunia Umoja wa Mataifa unafanya kazi na mashirika ya kikanda. Pichani ni Bankole Adeoye, Kamishna wa Umoja wa Afrika anayeshughulikia Masuala ya Kisiasa, Amani na Usalama, akitoa taarifa katika mkutano wa Baraza la Usalama kuhusu kuimarisha ushirikiano kati ya Umoja wa Mataifa na Muungano wa Afrika katika masuala ya amani na usalama barani Afrika, ikiwemo jukumu la Ofisi ya Umoja wa Mataifa katika Muungano wa Afrika, chini ya mada ya ushirikiano kati ya Umoja
Mbali ya mikusanyiko mingine mingi, ndani ya Umoja wa Mataifa kuna Baraza la usalama ambalo lina jukumu la kuhakikisha dunia ipo salama. Mbali ya kukaa katika vikao wajumbe hao wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa hufanya ziara mbalimbali na pichani wajumbe hao walizuru nchini Lebanon ikiwa ni sehemu ya ziara yao ya kusisitiza tena uungaji mkono kwa utulivu wa Lebanon na kutathmini maendeleo kuhusiana na Azimio namba 1701. Aliyeketi wa pili kutoka kushoto ni Jérôme Bonnafont, Mwakilishi wa Kudumu wa Ufaransa katika Umoja wa Mataifa, na upande wa kulia ni Claudia Banz, Mkurugenzi wa Kitengo cha Masuala ya Baraza la Usalama katika Idara ya Masuala ya Kisiasa na Ujenzi wa Amani (DPPA).
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa huteuwa wasaidizi wake katika maeneo mbalimbali ambao huitwa “Naibu Katibu Mkuu… wa eneo Fulani” kama vile Operesheni za ulinzi wa amani, mawasiliano ya Umma na masuala ya vijana.
Pichani Jean-Pierre Lacroix (kulia), Naibu Katibu Mkuu anayeshughulikia Operesheni za Kulinda Amani, anazungumza na mwanahabari wakati wa ziara yake mjini Juba alipotembelea vikosi vya usalama wa Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini (UNMISS).
Wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa wapo binadamu na pia wanayama ambao wana majukumu mbalimbali kama vile usalama na wengine husaidia kwenye hisia. Pichani Afisa Usalama wa Umoja wa Mataifa Gonzalez na mbwa wake mshirika, Hana, wanapiga picha katika siku ya pili ya mjadala wa Kikao cha 80 cha Baraza Kuu katika Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa. UNGA80