Wiki yenye shughuli nyingi zaidi ndani ya Umoja wa Mataifa ilianza kwenye Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani siku ya Jumatatu.
Zaidi ya Wakuu 110 wa Nchi na Serikali wanatarajiwa kukutana kwenye eneo hili la kimataifa lililoko katikati ya kitongoji cha Manhattan, New York.
Hii ilikuwa hotuba ya mwisho ya Mjadala Mkuu kwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, António Guterres, ambaye anatarajiwa kukamilisha ng’we yake mwishoni mwa mwaka huu. Alipigiwa makofi huku wajumbe kutoka sehemu mbalimbali za dunia wakisimama kwa heshima.
Takribani wajumbe 18,000 walitarajiwa kuhudhuria Mjadala Mkuu pamoja na zaidi ya matukio 160 yaliyopangwa kufanyika wakati wa wiki ya mikutano ya ngazi ya juu, (ingawa haijulikani ni yapi kati ya hayo yaliyofurahiwa na mshiriki huyu mchanga).