Joyce Msuya akiwa wilaya ya Mocímboa da Praia, Cabo Delgado, Msumbiji, Novemba 2023 akiwasikiliza mwanachama wa chama cha wanawake wa eneo hilo ambao waliathiriwa na mzozo na sasa wanajenga upya maisha yao kupitia mafunzo ya stadi za maisha.
Naibu Mratibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa wa misaada ya kibinadamu na masuala ya dharura Joyce Msuya akihutubia Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa jijini New York Marekani tarehe 26 Oktoba 2024 kuhusu majeshi ya Israel na kile wanachokifanya huko Ukanda wa Gaza eneo la Palestina linalokaliwa kimabavu na Israel.
Naibu Mkuu wa Masuala ya Kibinadamu na Naibu Mratibu wa Misaada ya Dharura Joyce Msuya alikutana na wafanyakazi wa OCHA nchini Colombia tarehe 16 May 2023 ili kupata ufahamu zaidi kuhusu utendaji kazi wao, maoni, mahitaji na wasiwasi wao na pia alizungumza nao kuhusu Mkakati wa OCHA kwa wafanyakazi wake na vipaumbele vya OCHA.