Haijalishi wapo wapi juhudi za kufikia kila mwananchi zinafanyika, na hapa wafanyakazi wa WHO wakishusha maboksi yenye vifaa tiba kutoka kwenye gari ili waingize kwenye boti litakalo safirisha kupeleka katika vituo vya afya na maeneo mengine yaliyotengwa maalum kutibu Ebola yanayofikika kwa boti.
© WHO
Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa Kulinda Amani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC (MONUSCO) umeviwezesha vituo vinne vya redio katika jimbo la Ituri, kaskazini mashariki mwa nchi, kwa mifumo ya nishati ya jua au sola na vifaa vya utangazaji ili kuboresha upatikanaji wa taarifa sahihi na kupambana na upotoshaji wa habari katika maeneo yaliyoathiriwa na changamoto za usalama na mlipuko wa Ebola.
©MONUSCO