Nchini Somalia, wanawake wengi wamekuwa wakiteseka kimya kimya kwa miaka mingi kufuatia majeraha wanayopata baada ya kujifungua. Shughuli za UNFPA zinazolenga utoaji wa upasuaji wa fistula zimesaidia wanawake hawa kujirudishia utu wao na kuungana tena na familia na jamii zao.
Hayat Peter (kulia) ni muuguzi ambaye amejitoa kwa miaka 22 kupigana dhidi ya fistula nchini Sudan Kusini. Kama muuguzi aliyejitolea, amewasaidia wanawake wengi kujirudishia heshima yao — kila kisa ikiwa ushindi mpya dhidi ya ugonjwa huu unaoweza kutibika
Kodi Moumdau alikimbilia Kituo cha Kituo cha Kitaifa cha Fistula kilichopo nje kidogo ya Niamey nchini Niger. Vituo kama hivi ni matumaini kwa wanawake wanaotafuta matibabu vinawapa usalama, huduma bora, na mazingira ya kupona kwa amani na heshima kamili.
Simulizi ya kutia matumaini kutoka nchini Bangladesh ambako kampeni ya miongo miwili ya UNFPA duniani ya kutokomeza fistula imezaa matunda kwa binti wawili wa Banessa Bibi (Katikati) ambao ni Jamena na Jamila. Walipata fistula ya uzazi lakini upasuaji umerejesha tabasamu kwenye nyuso zao, Wameondokana na aibu.