Anna, miongoni mwa makumi ya maelfu ya wakimbizi kutoka jimbo la Kordofan nchini Sudan, ameieleza UNFPA, jinsi yeye na watoto wake walivyokimbia bila kitu chochote zaidi ya maisha yao hadi kambini Abu Al Naja huko Gedaref, huku wakikwepa risasi zilizouwa mwenzao msituni na kupotezana na mume wake.
© UNFPA
UNFPA inasaidia timu ya madaktari inayotumia gari kutoa huduma katika kambi ya Abu Al Naja. Wanatoa huduma za afya ya mwili na akili, dawa muhimu zikiwemo zile za kusaidia manusura wa ubakaji, na pia kuna wakunga wanaohakikisha wajawazito wanapata huduma kabla na baada ya kujifungua.
© UNFPA