Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres akitoa maoni katika mkutano wa pembezoni mwa CSW70 uliowakutanisha wadau wa Asasi za Kiraia kutoka katika nchi mbalimbali.
Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Amina Mohammed (wa pili kutoka kushoto) alikutana na Ujumbe wa Asasi za Kiraia kutoka nchini Nigeria kandoni mwa CSW70 kujadili Muswada wa Viti Maalum kwa Wanawake Bungeni nchini Nigeria.
Nelly Mbangu Lumbulumbu, (Kulia) mwanasheria na mtetezi wa haki za binadamu kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) akihojiwa na Flora Nducha wa Idhaa ya Kiswahili ya UN na kufafanua jinsi shirika lake la Sauti ya Mama Mkongomani linavyowapigania wanawake Mashariki mwa DRC wakioathirika na vita kupata haki zao kisheria na kuhakikisha sauti zao zinasikika
Akihojiwa na Leah Mushi wa idhaa ya Kiswahili ya UN, Chausiku Kafuti Kuya (kulia) ambaye ni Naibu Mrajisi Mahakama Kuu Zanzibar nchini Tanzania amesema wamejenga na kuboresha mahakama kila wilaya ambazo zinatoa fursa kwa wananchi kuhudhuria kwa njia ya mtandao na pia wameweka vyumba maalum kwa ajili ya wanawake wanaonyonyesha na maeneo ya watoto kucheza ikiwa ni juhudi za kuhakikisha wanawake wanaenda mahakamani kutafuta haki bila vikwazo.
Zahra Salehe, Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la ICCAO katika mahojiano na Anold Kayanda wa Idhaa ya Umoja wa Mataifa Jijini New York, Marekani akieleza kuwa Mkutano wa 70 wa Kamisheni ya Hali ya Wanawake duniani, CSW70 kwake umekuwa jukwaa la kupigania vijana wapate kiti kwenye meza ya uamuzi kote duniani.
Rais wa Muungano wa Mabunge duniani, Dkt. Tulia Ackson (kulia) akizungumza na Assumpta Massoi wa Idhaa ya Umoja wa Mataifa kuhusu jinsi kikao alichoongoza kando wakati wa CSW70 kilichoangazia umuhimu wa kubadili Katiba, sheria na tamaduni ili kuendeleza haki za wanawake na wasichana.
Kutoka shirika la Kiraia la Jukwaa la Maendeleo ya Wanawake, Demokrasia na Haki, FODDAJ nchini Kenya ni Gertrude Micheni (kulia) Mwenyekiti wa Bodi na Salome Araka, mjumbe wa Bodi wa FODDAJ walifika ghorora ya 11 ya jengo la makao makuu ya Umoja wa Mataifa kuelezea ni kwa vipi wamenufaika na CSW70.