
Kuondoa unyanyasaji wa kijinsia katika ubunifu na matumizi ya Akili Mnemba au AI huanza kwa kutanguliza usawa wa kijinsia kama lengo, wakati ubunifu wa mifumo ya AI. Wasichana na wanawake wakishiriki katika sayansi hutoa mchango mkubwa katika nyanja hizi za teknolojia.

"Bado nakiona kisu, na yule mwanamke aliyenishikilia chini," anasema Hawa'a Mohamed Kamil. Sasa ana umri wa miaka 30, alikeketwa akiwa na umri wa miaka sita tu - uzoefu ambao haukuacha tu makovu ya kimwili lakini pia ya kisaikolojia. Sasa anaongoza harakati dhidi ya ukeketaji nchini mwake Djibouti.

Ushiriki wa wanawake kwenye michakato ya amani, kuanzia kwenye meza za kupanga mikakati hiyo, ni muhimu mathalani Sudan Kusini ambako (UNMISS) na washikadau wakuu walifanya kongamano la pamoja mwaka jana ili kuchunguza mikakati ya kukuza uongozi wa wanawake katika michakato ya kisiasa, amani na kidemokrasia.

Majanga yatokanayo na mabadiliko ya tabianchi yanapotokea, ukatili wa kingono dhidi ya wanawake nao hushamiri. Ndio maana wataalamu wa shirika la Umoja wa Mataifa la Afya ya Uzazi na Idadi ya Watu (UNFPA) nchini Nigeria linaelimisha wakimbizi hapa Maiduguri, jinsi ya kujikinga na ukatili wa kijinsia unaoweza kuwakumba.

Hawa ni makungwi wa ndoa za kimila nchini Zambia. Kupitia mafunzo yaliyotolewa na UNFPA nchini Zambia, sasa wanahakikisha hakuna msichana anaolewa akiwa na umri wa chini ya miaka 20, hata baada ya Bunge kupitisha sheria ya kupiga marufuku ndoa za kiserikali, kimila na kidini kwa watoto wa kike wenye umri wa chini ya miaka 18.