Upper Nile hali si shwari, watoto wakimbia bila mwongozo
Nchini Sudan Kusini mapigano ya kikabila kwenye jimbo la Upper Nile nchini humo yamesababisha vifo, ukimbizi wa ndani halikadhalika madhila zaidi kwa watoto ambao mustakabali wao unazidi kuwa mashakani huku nao wazee wakishuhudia machungu katika taifa hilo changa zaidi duniani.