Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Chuja:

Somalia

Pwani ya Mogadishu, nchini Somalia
UNODC/Jeremy Douglas

Viongozi wa OCHA na FAO kuadhimisha siku ya wanawake duniani nchini Somalia

Ziara ya Naibu Mkuu wa Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Kuratibu Misaada ya Kibinadamu na Masuala ya Dharura OCHA Bi. Joyce Msuya na Naibu Mkurugenzi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo FAO Beth Bechdol nchini Somalia imewaonesha namna takriban watu milioni 7 walivyo na uhitaji wa msaada wa haraka wa kuokoa maisha kutokana na kuathirika na njaa, vita na mabadiliko ya tabianchi.