Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Chuja:

Rohingya

Mama na binti yake wakisubiri kutua kwa kimbunga Mocha kwenye makazi ya warohingya huko Cox's Bazaar nchini Bangladesh.
© UNICEF/Suman Paul Himu

Miaka 6 ya mateso kwa warohingya; Jamii ya kimataifa msiwasahau- Türk

Ikiwa kesho ni miaka 6 tangu serikali ya kijeshi nchini Myanmar ianze msako wa kufurusha waislamu wa kabila la Rohingya kutoka jimbo la Rakhine nchini humo, Kamishna Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu Haki za Binadamu Volker Türk amesema jamii ya kimataifa isisahau warohingya na wale wanaowahifadhi, na zaidi ya yote juhudi za kimataifa ziongezwe maradufu ili wahusika wawajibishwe.