Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Chuja:

DR Congo

Wanawake wanakabiriwa na changamoto kuwaepusha watoto wao na ugonjwa wa Bubonic katika maeneo ya Ituri, DRC.
© UNICEF/Scott Moncrieff

Mlipuko wa Bubonic unahatarisha maisha ya watoto Congo DRC: UNICEF

Kuibuka tena kwa ugonjwa wa Bubonic unaosambazwa na viroboto kutoka kwa wanyama kama panya na nguchiro kwenda kwa binadamu baada ya kuwauma na kisha binadamu aliyeambukizwa kuweza kuambukiza binadamu mwingine, kunaweka maisha ya watoto na vijana hatarini, katika jimbo la Ituri Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC)  limeonya leo shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF. 

Mkimbizi wa ndani nchini Msumbiji akipokea msaada wa chakula
© WFP/Grant Lee Neuenburg

Kuisaidia WFP ni kuwasaidia wakimbizi kama Adu

Mkimbizi wa ndani Abbas Adu na wengine 400,000 wamelishukuru Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa chakula WFP kuwapatia msaada wa chakula wakati huu ambapo WFP imepaza sauti kwa wahisani kusaidia wananchi Milioni 41 wanaokabiliwa na njaa kutokana na hali mbaya ya hewa ambayo imeathiri mavuno yao na hivyo kukosa chakula.

Sauti
2'2"
Jeanne Lusungi ambaye ni muuguzi katika hospitali ya jimbo la Kivu Kaskazini nchini DRC akimpatia chanjo ya kwanza askari huko DRC.
UNICEF/Arlette Bashizi

Ninafurahi sana wagonjwa wanaporejea kunishukuru- Muuguzi Jeanne

Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa hii leo limezindua rasmi mwaka huu wa 2021 kuwa mwaka wa kimataifa wa wahudumu wa afya na wanaohudumia wagonjwa ikiwa ni kutambua mchango wao katika kukabiliana na ugonjwa wa Corona au COVID-19 ambapo katika kutambua hilo, tunammulika muuguzi Jeanne Lusungu kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC ambaye makuzi yake yalikuwa chachu ya kufanya kazi yake ya sasa.