DRC: Mapigano yameshamiri tangu kumalizika kwa uchaguzi mkuu Desemba- Keita
Hali ya usalama mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC imezorota tangu kukamilika kwa uchaguzi mkuu nchini humo mwishoni mwa mwezi Desemba mwaka jana, amesema Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini humo, Bintou Keita wakati akihutubia Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa hii leo.