UNGA80
Pazia la Mjadala Mkuu UNGA80 lafungwa kwa wito wa uwiano wa uwakilishi, mageuzi na hatua za pamoja
Siku sita za Mjadala Mkuu wa Mkutano wa 80 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa (UNGA80) zimetamatika leo Jumatatu Septemba 29 alasiri kwa Rais wa Baraza hilo Annalena Baerbock kuhutubia na kusisitiza umuhimu wa uwakilishi wa kimataifa, mshikamano, na kasi ya kufanyia mageuzi chombo hicho katika dunia inayobadilika kwa kasi.
Vatican yasisitiza amani, upokonyaji silaha na heshima kwa ubinadamu: UNGA80
Vaticani ametoa wito mzito wa mshikamano wa kimataifa, amani na haki wakati wa Mjadala Mkuu wa Mkutano wa 80 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, ambapo Askofu Mkuu Paul Richard Gallagher, Katibu wa Uhusiano na Mataifa wa Vatican, ameonya kuwa dunia ipo katika njia panda ya hatari.
Malawi: Ushiriki wa wanawake katika operesheni za ulinzi wa amani ‘unalipa’
Malawi katika Mjadala Mkuu wa mkutano wa 80 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa imewakilishwa na Balozi Agnes Mary Chimbiri-Molande ambaye amezungumzia maendeleo ambayo nchi yake imepiga katika kukuza usawa wa kijinsia na ushiriki wa wanawake katika operesheni za ulinzi wa amani.
Burundi imefunga ukusara wa machafuko na kufungua wa maridhiano: Bizimana
Katika hotuba yenye nguvu katika kikao cha 80 cha Mjadala Mkuu wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, UNGA80 Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kikanda wa Burundi, Balozi Edouard Bizimana, amethibitisha ahadi ya nchi yake kwa suala la amani, maendeleo, na haki za binadamu huku akiutaka Umoja wa Mataifa kufanya marekebisho ya dharura ili kuendana na changamoto za dunia ya sasa. Akimwakilisha Rais Evariste Ndayishimiye, Bizimana amesisitiza nafasi muhimu ya ushirikiano wa kimataifa katika kukabiliana na migogoro ya kidunia.
Zambia: Kama hakuna utulivu katika eneo moja, hakuna utulivu kila mahali
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa Zambia, Mheshimiwa Mulambo Haimbe, ambaye amesema Zambia inalaani vikali vita na uvamizi na wanasihi pande zote kwenye mizozo iliyotawala duniani kuchagua diplomasia badala ya vita.
Wakati wa Afrika kupewa viti na sauti Baraza la Usalama la UN ni sasa: Lokaale
Mwakilishi wa kudumu wa Kenya katika Umoja wa Mataifa, Balozi Ekitela Lokaale, amesema kuwa ni wakati muafaka kwa Afrika kupewa nafasi ya kudumu katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, ili bara hilo liwe na sauti sawa na mataifa makubwa katika uamuzi wa masuala ya amani na usalama duniani.
Ili Afrika ‘iimarike kiafya’ inabidi isiwe tegemezi kwenye masuala ya kifedha - Dkt. Ntuli Kapologwe
Tukisalia hapa katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa, kandoni mwa Mjadala Mkuu wa Mkutano wa 80 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, UNGA80, inafanyika mikutano mingine ya pembezoni kujadili masula mengine ya kusongesha maendeleo ya ulimwengu. Wiki iliyopita tulizungumza na Dkt. Ntuli Kapologwe Mkurugenzi Mkuu wa Jumuiya ya Afya ya Mashariki, Kati na Kusini mwa Afrika, ECSA wakati alipokuwa akisubiri kushiriki mkutano wa nchi wanachama wa jumuiya hiyo kujadili jinsi ya kusongesha diplomasia ya kisayansi ili kuhakikisha bara la Afrika haliachwi nyuma kwenye kukabiliana na changamoto za kiafya.
Eritrea: Lazima kuwe na mpangilio mpya wa dunia uliojikita katika haki na usawa
Waziri wa Mambo ya Nje wa Eritrea, Osman Saleh Mohammed, amehutubia Mjadala Mkuu wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa katika Kikao cha 80 au UNGA80, akionya kwamba mfumo wa sasa wa ulimwengu unaainishwa na “utawala wa kikatili, ujambazi, udanganyifu na ukandamizaji.”
NUKUU ZA VIONGOZI: Mjadala Mkuu wa Baraza Kuu la UN, UNGA80- SIKU YA SITA
Mjadala Mkuu wa mkutano wa 80 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa leo ni siku ya sita ambapo viongozi wa dunia wanaendelea kutoa hotuba zao kwenye ukumbi wa Baraza Kuu kuhusu yale waliyofanya kusongesha amani, haki za binadamu na maendeleo duniani. Kila kiongozi wa nchi 193 wanachama wa Umoja wa Matiafa atapata fursa ya kuhutubia kwenye mjadala huo utakaofikia tamati tarehe 29 Septemba. Bofya hapa kupata ratiba. Mjadala huanza saa 3 asubuhi kwa saa za New York, Marekani hadi saa 3 usiku. Tazama Mubashara hapa.
Kando ya hotuba hizo, wanashiriki vikao vya kando vinavyomulika masuala kama vile afya, amani na usalama duniani.