UNGA80
UNGA80 na maelezo kuhusu magonjwa yasiyo ya kuambukiza NDCs - Dkt. Mohamed Yakub Janabi
Mada hii kwa kina inamulika mkutano wa ngazi ya juu kuhusu magonjwa yasiyo ya kuambukiza NDCs unaoendelea kandoni mwa Mjadala Mkuu wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa UNGA80. Flora Nducha wa Idhaa hii amepata fursa ya kuzungumza na mmoja wa wazungumzaji wa Mkutano huo Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Afya la Umoja wa Mataifa WHO Kanda ya Afrika Dkt. Mohamed Yakub Janabi
Nyuklia ni tishio kubwa la kimataifa linaloongezeka: UN
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa leo ameonya mbele ya wajumbe wa mkutano wa ngazi ya juu kando ya Mjadala Mkuu wa Umoja wa Mataifa UNGA80 mjini New York unaojadili kuondoa silaha za nyuklia kuwa “tishio hilo linaendelea kuwa hatari kubwa ya kimataifa.”
Kutokomeza silaha za nyuklia badala ya uharibifu: Msukumo mpya kwa dunia isiyo na silaha za nyuklia
Silaha za nyuklia bado zinabaki kuwa mojawapo ya vitisho hatari zaidi kwa ubinadamu. Viongozi wa dunia wanatathmini tena hatari kubwa zinazoletwa na silaha hizi na wanasisitiza juhudi mpya za kimataifa za kuziangamiza kabisa katika Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa Ijumaa hii.
UNGA80:Hotuba ya Netanyahu yakumbana na upinzani, yeye augeuza ukumbi kuwa darasa
China yataka mshikamano huku ikiahidi msaada zaidi kwa UN
Waziri Mkuu wa China, Li Qiang, leo aonya katika Mjadala Mkuu wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kwamba dunia imeingia katika kipindi kipya cha mizozo na mabadiliko, huku sera za upande mmoja na mtazamo wa vita baridi zikirejea.
26 SEPTEMBA 2025
Hii leo ni hotuba ya Israeli kwenye mjadala mkuu wa baraza kuu, nini kilitokea? Kijana daktari mwanaharakati kutoka Ghana aishiye Uingereza akiwa UNGA80 na matumaini mapya ya kinga dhidi ya maambukizi ya VVU.
Hotuba ya Netanyahu yakumbana na upinzani, yeye augeuza ukumbi kuwa darasa
Mjadala Mkuu wa Mkutano wa 80 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa ukiwa umeingia katika siku yake ya nne hapa kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani leo Ijumaa, Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu amekuwa wa kwanza kuzungumza akitumia muda wake mwingi kushambulia wanamgambowa kipalestina, Hamas na kutetea kila uamuzi wa Israel. Anold Kayanda ameifuatilia hotuba hiyo kwa kina.
Makamu wa Rais wa Uganda atoa wito wa ushirikiano wa kimataifa na amani katika UNGA80
Makamu wa Rais wa Uganda, Meja Mstaafu Jessica Alupo, akihutubia Kikao cha 80 cha Mjada Mkuu wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa jijini New York siku ya Alhamisi, ametoa wito kwa jumuiya ya kimataifa kuimarisha ushirikiano wa kimataifa na kuongeza juhudi za kudumisha amani, maendeleo na haki za binadamu.
Ni wakati wa sauti zetu vijana zisikilizwe kwa vitendo: Mwanaharakati Dkt.Owusu
Katika Mkutano wa Vijana wa Umoja wa Mataifa unaofanyika kandoni mwa mjadala mkuu wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa UNGA80 unaoendelea hapa New York, viongozi vijana kutoka duniani kote wanataka uwakilishi mkubwa katika maamuzi ya kimataifa.