Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNGA80

Mkutano wa Baraza Kuu - Taarifa Maalum ya UNGA80
23 Septemba – 30 Septemba 2025
Jukwaa limewekwa tayari kwa ajili ya Mjadala Mkuu wa Mkutano wa 80 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa.
Mkutano huu utafunguliwa chini ya kaulimbiu “Bora Pamoja: Miaka 80 na Zaidi kwa Amani, Maendeleo na Haki za Binadamu”, ikiwa ni hatua muhimu inayofanyika katikati ya changamoto kubwa duniani na wito wa dharura wa kuchukua hatua mpya za ushirikiano wa kimataifa.
Mjadala wa Ngazi ya Juu utaanza rasmi tarehe 22 Septemba kwa siku nzima ya mikutano ya kilele na maadhimisho, ikiwemo kumbukumbu ya miaka 80 tangu kuanzishwa kwa Umoja wa Mataifa, tukio la wakati wa Malengo ya Maendeleo Endelevu au SDG Moment na kutimia miaka 30 tangu Mkutano wa Dunia wa Beijing kuhusu wanawake. Viongozi pia watashiriki kwenye mkutano wa ngazi ya juu kuhusu Suluhu ya amani kwa suala la Palestina na utekelezaji wa suluhu ya mataifa mawili.
Kuanzia tarehe 23 hadi 29 Septemba, macho na masikio ya dunia yatageukia jukwaa maarufu lenye marumaru ya kijani ndani ya Ukumbi wa Baraza Kuu, ambapo marais, mawaziri wakuu na wafalme watawasilisha taarifa za kitaifa, wakibainisha dira zao kuhusu amani, maendeleo, haki za binadamu na hatua za pamoja wakati huu wa changamoto zinazoongezeka duniani.
Ajenda pia itahusisha mkutano wa kilele unaofanyika kila baada ya miaka miwili kuhusu ufadhili wa maendeleo endelevu, Mkutano wa Tabianchi, uzinduzi wa Mazungumzo ya kimataifa kuhusu Usimamizi wa Akili Mnemba AI, Hatua za dunia kuhusu magonjwa yasiyoambukiza NDCs na afya ya akili, pamoja na hali ya Waislamu Warohingya na wengine walio wachache nchini Myanmar.
Hapa, Idhaa ya Kiswahili inakupa fursa ya kuketi mstari wa mbele kushuhudia yote yanayojiri. Kupitia simu yako ya rununu au kompyuta, fuatilia Wakuu wa Nchi na Serikali wanapojadili masuala makubwa ya wakati wetu na kuelekeza dira ya taswira mpya ya Umoja wa Mataifa.
 
Tembelea majukwaa yetu ya mitandao ya kijamii: Youtube: Habari za UN X: Habari za UN
Rais Volodymyr Zelensky wa Ukraine akihutubia mjadala mkuu wa kikao cha themanini cha Baraza Kuu.
UN Photo/Loey Felipe

Ukraine: Taasisi za kimataifa zimekuwa dhaifu

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy amesema taasisi za kimataifa zimekuwa dhaifu wanachoweza kufanya ni kutoa matamko makali pekee na kwamba kwa sasa duniani sheria pekee za Kimataifa haziwezi kusaidia nchi kujilinda bila ya kuwa na silaha pamoja na marafiki wenye nguvu wa kukusaidia. 

Sauti
3'4"
© UNICEF/Oleksii Filippov

Taasisi za kimataifa zimekuwa dhaifu - Volodymyr Zelenskyy

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy amesema taasisi za kimataifa zimekuwa dhaifu wanachoweza kufanya ni kutoa matamko makali pekee na kwamba kwa sasa duniani sheria pekee za Kimataifa haziwezi kusaidia nchi kujilinda bila ya kuwa na silaha pamoja na marafiki wenye nguvu wa kukusaidia. Tupate taarifa zaidi kutoka kwa Leah Mushi.

Sauti
3'4"
UN Video

ECSA: Diplomasia ya kisayansi kutumika kusongesha Mkataba wa Zama Zijazo Afrika

Katika siku ya pili ya Mjadala Mkuu wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, UNGA, kando ya hotuba, viongozi wa nchi 9 wanachama wa Jumuiya ya Afya ya Mashariki, Kati na Kusini mwa Afrika, ECSA watakuwa na mkutano wa kusongesha diplomasia ya kisayansi ili kuhakikisha bara la Afrika haliachwi nyuma kwenye kukabiliana na changamoto za kiafya, baada ya kujifunza kutokana na COVID-19 au UVIKO19. Mkurugenzi Mkuu wa ECSA Dkt. Ntuli Kapologwe akihojiwa na Assumpta Massoi wa Idhaa hii ametaja wanachotarajia kwenye mkutano huo..

Sauti
7'23"