UNGA80
Tambueni kinachoendelea Mashariki mwa DRC kuwa ni mauaji ya halaiki - Tshisekedi
Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Félix-Antoine Tshisekedi Tshilombo, amehutubia mkutano wa 80 wa Mjadala Mkuu wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa (UNGA80) jijini New York, Marekani na kusema kwamba vita dhidi ya ukosefu wa haki, ubaguzi na ufisadi ni muhimu ili kuzuia migogoro, akikumbusha kuwa makubaliano ya amani hayawezi kuwa ya mafanikio bila hakikisho la haki na usaidizi kwa manusura.
Angola: UN lazima ifanye mageuzi kwani dunia ina chaguzi mbili, kati ya amani na vita
Rais wa Angola na Mwenyekiti wa Muungano wa Afrika João Manuel Gonçalves Lourenço ametumia hotuba yake katika Kikao cha 80 cha Mjadala wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kutoa onyo kali, “dunia imesimama mbele ya uchaguzi wa kufanya kila kitu ili kulinda amani au kukabiliana na vita na madhara yake yote, hivyo kuhatarisha mustakabali wa ubinadamu.”
Afrika Kusini: Umefika wakati wa UN kuongozwa na mwanamke
Afrika Kusini imesema umefika wakati wa Umoja wa Mataifa kuongozwa na mwanamke na kwamba nchi hiyo inaunga mkono uchaguzi wa kiongozi mwanamke kushika wadhifa wa juu zaidi wa taasisi hiyo kubwa zaidi duniani
Mkwamo kwenye Baraza la Usalama ni chachu ya UN kutotimiza lengo la amani duniani: Lokaale
Umoja wa Mataifa mwaka huu umeadhimisha miaka themanini tangu kuanzishwa kwake baada ya Vita Kuu ya Pili ya Dunia, lengo likiwa kuhakikisha dunia inabaki mahali salama na pasipo vita. Hata hivyo, changamoto za amani duniani zinaibua maswali juu ya ufanisi wake.
Marekani yajinasibu kwa mafanikio ya kumaliza migogoro isiyokwisha
Rais wa Marekani – Donald J. Trump akihutubia Mjadala Mkuu wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kikao cha 80 hii leo jijini New York amejinasibu kwamba amefanikiwa kumaliza mogogoro siyokwisha “Katika kipindi cha miezi saba, nimemaliza vita saba ambavyo havikuisha “amedai Rais huyo.
UN yajipanga kuhakikisha Dunia inapata habari bila mkwamo
Mjadala Mkuu wa Mkutano wa 80 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa ukianza rasmi hii leo katika Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York Marekani zaidi ya watu 40,000 wanatarajiwa kuunganishwa kwenye mtandao wa intaneti (Wi-Fi) kusikiliza kile kitakachoelezwa na viongozi wa ngazi za juu, pamoja na wakuu wa nchi na serikali.
Brazil: Umaskini ni adui wa demokrasia kama vile ulivyo ugaidi
Vita pekee ambayo kila mtu anaweza kushinda ni ile tunayopigania dhidi ya njaa na umaskini amesema Rais wa Brazil Luiz Inácio Lula Da Silva, akihutubia leo Mjadala Mkuu wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa Jijini New York.
Guterres: Umoja wa Mataifa ni ngao ya binadamu, tusichague kukata tamaa
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ametoa wito kwa dunia kufanya maamuzi ya lazima kuhusu mustakabali wake, akisema kuwa miaka 80 tangu kuanzishwa kwa Umoja wa Mataifa ni fursa ya kuamua “ni aina gani ya dunia tunataka kujenga pamoja.”
23 SEPTEMBA 2025
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina maalum na mada yetu inamulika maoni kuhusu miaka 80 ya Umoja wa Mataifa. Pia tunakuetea muhtasari wa habari unaofuatilia ujumbe wa viongozi katika mjadala mkuu wa UNG80.
Huu ni wakati wa hatua na si wa sherehe kurejesha hadhi ya UN: Baerbock
Akikumbuka miaka 80 ya Umoja wa Mataifa, Rais wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa Annalena Baerbock leo amefungua Majadiliano Mkuu wa Batraza Kuu UNGA80 kwa kuwakumbusha nchi wanachama kwamba wakati huu “sio mwaka wa kawaida na sio wakati wa sherehe, bali ni kwa kutafakari juu ya kushindwa kwa taasisi na umuhimu wake endelevu.”
Pagination
- 1
- 2