UNGA80
Mkutano wa UN wasukuma suluhisho ya mataifa mawili wakati mataifa zaidi yakitambua Palestina
Mkutano wa ngazi ya Juu wa kimataifa kuhusu utatuzi wa amani wa suala la Palestina umefunguliwa leo katika Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York, chini ya uenyekiti wa pamoja wa Ufalme wa Saudi Arabia na Ufaransa.
Miaka 30 ya Azimio la Beijing, Umoja wa Mataifa washerehekea mafanikio katika haki za wanawake
Kumekuwa na maendeleo, lakini changamoto nyingi bado zipo, hii ndiyo msingi mkuu wa hotuba zilizotolewa katika mkutano wa ngazi ya juu wa kuadhimisha miaka 30 ya Azimio la Beijing kuhusu Haki za Wanawake leo katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani.
Mkutano wa mabadiliko ya tabianchi 2025 ni njia kuelekea COP30
Mafuriko Kusini mwa Asia, moto wa nyika Amerika Kaskazini, na joto la kihistoria barani Ulaya vimeonesha kile ambacho wanasayansi wameonya kwa miaka mingi, mabadiliko ya tabianchi yanazidi kasi kuliko hatua za kisiasa za kuyakabili.
Umoja wa Mataifa waadhimisha miaka 80 tangu kuanzishwa kwake
Umoja wa Mataifa hii leo umeadhimisha miaka 80 tangu kusainiwa kwa Mkataba wake tarehe 26 Juni 1945, tukio lililotoa matumaini mapya kwa dunia iliyokuwa imechoka kutokana na vita kuu mbili za dunia, mauaji ya halaiki na ukoloni. Katika maadhimisho hayo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres amesema kumbukizi ya kuanzishwa kwa Umoja wa Mataifa ni fursa ya kukumbuka ujasiri wa waanzilishi wa taasisi hiyo na kuimarisha mshikamano wa kimataifa katika kukabili changamoto zinazokabili dunia hivi sasa.
Tumefika hapa UN, tafadhali tusikilizeni
Kando ya maadhimisho ya siku ya miaka 80 ya Umoja wa Mataifa, hapa makao makuu kumefanyika mashauriano ya faragha yenye lengo la kusaka majawabu ya madhara ya mabadiliko ya tabianchi. Mashauriano ya leo ni sehemu ya mashauriano 10 yatakayofanyika kuelekea mkutano wa tabianchi wa wakuu wa nchi na serikali utakaofanyika keshokutwa Jumatano hapa Umoja wa Mataifa.