UNGA80
Dunia ndani ya jengo moja la UN: Unachopaswa kufahamu kuhusu UNGA80
Viongozi wa dunia wanakutana kwenye Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa, kandoni mwa tawi la Mashariki la mto Hudson, eneo la Manhattan, kitongoji cha New York, kwa kile kinachotazamwa kuwa moja ya mikutano muhimu ya mwaka katika zama za karibuni.
Mkuu wa UN aonya kuhusu migawanyiko ya kimataifa kabla ya Mkutano wa UNGA80
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, António Guterres, ametoa wito kwa viongozi wa dunia “kuwa makini na kutekeleza ahadi” wanapowasili jijini New York kwa ajili ya wiki ya ngazi ya juu ya Mkutano wa Baraza Kuu wa 80 wa Umoja wa Mataifa UNGA80.
Tumejipanga vema tayari kuhudumia UNGA80 - Kamishna wa Masuala ya Kimataifa wa jiji la New York, Marekani
Wakazi wa jiji la New York, Marekani wanakijua vyema kipindi hiki cha mwaka. Wageni huanza kuwasili jijini, usalama huimarishwa, na barabara hufungwa au kubadilishwa matumizi yake, hasa zile zinazoelekea ‘First Avenue’ ya Manhattan, ambako ndiko makao makuu ya Umoja wa Mataifa yalipo.
16 SEPTEMBA 2025
Jaridani leo jaridani tunakuletea mad akwa kina inayoangazia mjadala Mkuu wa mkutano wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa. Pia tunakuletea muhtasari wa habari na ufafanuzi wa neno la wiki.