Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNGA80

Mkutano wa Baraza Kuu - Taarifa Maalum ya UNGA80
23 Septemba – 30 Septemba 2025
Jukwaa limewekwa tayari kwa ajili ya Mjadala Mkuu wa Mkutano wa 80 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa.
Mkutano huu utafunguliwa chini ya kaulimbiu “Bora Pamoja: Miaka 80 na Zaidi kwa Amani, Maendeleo na Haki za Binadamu”, ikiwa ni hatua muhimu inayofanyika katikati ya changamoto kubwa duniani na wito wa dharura wa kuchukua hatua mpya za ushirikiano wa kimataifa.
Mjadala wa Ngazi ya Juu utaanza rasmi tarehe 22 Septemba kwa siku nzima ya mikutano ya kilele na maadhimisho, ikiwemo kumbukumbu ya miaka 80 tangu kuanzishwa kwa Umoja wa Mataifa, tukio la wakati wa Malengo ya Maendeleo Endelevu au SDG Moment na kutimia miaka 30 tangu Mkutano wa Dunia wa Beijing kuhusu wanawake. Viongozi pia watashiriki kwenye mkutano wa ngazi ya juu kuhusu Suluhu ya amani kwa suala la Palestina na utekelezaji wa suluhu ya mataifa mawili.
Kuanzia tarehe 23 hadi 29 Septemba, macho na masikio ya dunia yatageukia jukwaa maarufu lenye marumaru ya kijani ndani ya Ukumbi wa Baraza Kuu, ambapo marais, mawaziri wakuu na wafalme watawasilisha taarifa za kitaifa, wakibainisha dira zao kuhusu amani, maendeleo, haki za binadamu na hatua za pamoja wakati huu wa changamoto zinazoongezeka duniani.
Ajenda pia itahusisha mkutano wa kilele unaofanyika kila baada ya miaka miwili kuhusu ufadhili wa maendeleo endelevu, Mkutano wa Tabianchi, uzinduzi wa Mazungumzo ya kimataifa kuhusu Usimamizi wa Akili Mnemba AI, Hatua za dunia kuhusu magonjwa yasiyoambukiza NDCs na afya ya akili, pamoja na hali ya Waislamu Warohingya na wengine walio wachache nchini Myanmar.
Hapa, Idhaa ya Kiswahili inakupa fursa ya kuketi mstari wa mbele kushuhudia yote yanayojiri. Kupitia simu yako ya rununu au kompyuta, fuatilia Wakuu wa Nchi na Serikali wanapojadili masuala makubwa ya wakati wetu na kuelekeza dira ya taswira mpya ya Umoja wa Mataifa.
 
Tembelea majukwaa yetu ya mitandao ya kijamii: Youtube: Habari za UN X: Habari za UN
© WHO

Uhaba wa maji watishia mafanikio ya SDGs – Guterres

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, António Guterres, ameonya kwamba dunia ipo nyuma katika kutekeleza ahadi zake kuhusu upatikanaji wa maji safi na salama na huduma za kujisafi. Hivyo basi amezitaka serikali, sekta binafsi na jamii kuchukua hatua za haraka kukabiliana na uhaba unaoongezeka wa maji, uchafuzi wa mazingira na shinikizo linalotokana na mabadiliko ya tabianchi. Assumpta Massoi na maelezo zaidi.

Sauti
3'29"

01 JULAI 2026

Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina. Ikiwa ni siku chache baada ya maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Watu Wasioona na viziwi inayoadhimishwa tarehe 27 Juni kila mwaka, Rashid Malekela wa Idhaa hii anakupeleka Mashariki ya Kati akimmulika mkazi mwenye ulemavu ambaye anakumbwa na changamoto katikati ya vita.

Sauti
9'58"

23 APRILI 2026

Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina ambapo juzi Jumanne na jana Jumatano wagombea wa nafasi ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa walipata fursa kunadi serra zao mbele ya nchi wanachama kwenye Baraza Kuu wakiwemo wawakilishi wa asasi za kiraia walioweza kuwauliza maswali. 

Miongoni mwa wawakilishi hao ni Irene Kitoti, Mwanzilishi na mkurugenzi wa asasi ya kiraia ya Genesis For Children Organization ya nchini Tanzania aliyezungumza na Flora Nducha wa Idhaa hii ya Kiswahili. Pia tunakuletea muhtasari wa habari kama zifuatazo.

Sauti
9'59"
UN News/Abdelmonem Makki

Akiwa Doha, Rais wa Baraza Kuu aona watoto wa kipalestina walivyo na matumaini licha ya zahma walizopita

Rais wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa Annalena Baerbock ametembelea wakimbizi wa kipalestina huko Doha nchini Qatar kuwajulia hali na kujionea maisha yao baada ya kuondolewa wakati wa vita kali huko Ukanda wa Gaza eneo la wapalestina linalokaliwa kimabavu na Israel na kuletwa nchini Qatar kwa ajili ya kupatiwa matibabu. Leah Mushi anatupa taswira ya ziara yake hiyo.

Sauti
4'6"
Kiongozi wa Timu ya Uwekezaji ya Kanda ya UNCDF kwa Afrika Mashariki na Kusini, Omon Ukpoma-Olaiya, anahojiwa na Anold Kayanda mbele ya ukuta wa kijani wenye nembo ya Malengo ya Maendeleo Endelevu UN katika UMOJA WA MATAIFA huko New York.
UN News

Namna UNCDF ilivyosaidia jamii kupata mtaji na huduma muhimu Rwanda, Burundi, Malawi na Zimbabwe

Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuendeleza Mitaji, UNCDF, limeendelea kuwekeza katika kupunguza hatari za hasara za kifedha na kufungua fursa za mitaji nafuu kwa vijana, wanawake na sekta muhimu barani Afrika. Hayo yanasemwa na Omon Ukpoma-Olaiya, Kiongozi wa Uwekezaji wa UNCDF kwa Kanda ya Afrika Mashariki, Kusini na Nchi za Kiarabu, alipokuwa akizungumza na Anold Kayanda na Anold Kayanda wa Idhaa ya Umoja wa Mataifa, jijini New York, Marekani kandoni mwa Mjadala Mkuu wa Mkutano wa 80 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa uliofikia tamati Septemba 29, 2025.

Ishara ya Umoja wa Mataifa kwenye sakafu ya Duka la Mkutano Mkuu.
UN Photo/Loey Felipe

Takwimu za UNGA: Hotuba ndefu zaidi, Wanawake Wachache, na baadhi kutokuwepo

Kwa muda wa siku sita, safu ya viongozi wa dunia (194 kwa jumla, 24 tu kati yao wakiwa ni wanawake) walitoa hotuba kwenye Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kutoka kwenye jukwaa lake la kuvutia la marumaru ya kijani kibichi, wakiangazia vita huko Jamhuri ya Kidemokrasia Congo, DRC, Sudan, Gaza na Ukraine, mzozo wa mabadiliko ya tabianchi, na mageuzi katika Umoja wa Mataifa, miongoni mwa masuala mengine mengi muhimu.

UN News

EAC yasisitiza usalama, uchumi na masuala ya kidijitali katika Mjadala Mkuu wa UNGA80

Kama unavyofahamu Mjadala Mkuu wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa UNGA80 umekunja jamvi rasmi  jana Jumatatu. Na tumepata fursa ya kuzungumza na washiriki mbalimbali akiwemo Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki EAC, Veronica Nduva ambaye alizungumza na Flora Nducha kandoni mwa mjadala huo kuangazia mchango wa Jumuiya ya Afrika Mashariki katika kutekeleza ajenda ya Umoja wa Mataifa ikiwemo masuala ya Amani na usalama, maendeleo na ushirikiano wa kikanda. Ungana nao.

Sauti
9'11"