Mkutano wa 74 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa unaanza mwezi huu wa Septemba hadi wiki ya pili ya mwezi Septemba mwakani. Katika ukurasa huu hata hivyo tutakuwa tunakuletea habari motomoto kutoka mjadala wa wazi na vikao vya ngazi ya juu vya mkutano huo ambavyo vinafanyika kuanzia tarehe 22 septemba 2019 hadi 30 Septemba 2019. Pamoja na hotuba za viongozi ni vikao vya ngazi ya juu kuhusu Mkutano wa vijana wa vijana na mabadiliko ya tabianchi, fursa ya afya kwa wote, mkutano kuhusu fursa ya afya kwa wote, tathimini ya hatua za utekelezaji wa malengo ya maendeleo endelevu, ufadhili kwa ajili ya maendeleo na tathimini ya mwelekeo wa mkakati wa SAMOA.
MKUTANO WA 74 WA BARAZA KUU LA UMOJA WA MATAIFA
25 Septemba 2019
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa awaeleza wajumbe wa mjadala wa Baraza la Umoja wa Mataifa kuwa hatua zimepigwa lakini bado wana kazi katika kutimiza haki za mtoto.
Tumepiga hatua lakini bado tuna kazi katika kutimiza haki za mtoto:Guterres
Tangu kupitishwa kwa mkataba wa haki za mtoto miaka 30 iliyopita pamoja na mafanikio makubwa yaliyopatikana kote duniani bado vita imesalia kuwa chanzo kubwa ya ukiukwaji wa haki za mtoto na bado kuna nchi hazijaridhia mkataba huo amesema Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres.
Tunaweza kufanya lolote iwapo tu majasiri- Profesa Bande
Rais wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa Profesa Tijjani Muhammad-Bande amerejea tena kauli yake ya kusihi ushirikiano wa kimataifa ili kuweza kunasua mamilioni ya watu kutoka lindi la umaskini.
Afrika ni chanzo cha masuluhisho, Rwanda tuko tayari kufanya sehemu yetu-Paul Kagame
Rais Paul Kagame wa Rwanda ameitumia hotuba yake katika mjadala mkuu wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, UNGA74 mjini New York hii leo, kueleza kuwa Afrika inaweza pia kuwa chanzo cha masuluhisho ya matatizo yanayoukabili ulimwengu.
Twahitaji ujasiri zaidi hivi sasa kuliko wakati wowote kutatua changamoto za dunia- Macron
Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron amehutubia mjadala mkuu wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa hii leo Jumanne jijini New York, Marekani akitaka mwelekeo wa kijasiri zaidi katika kutatua vitisho vikubwa vinavyokabili dunia hivi sasa.
Habari njema ni kwamba ajenda ya 2030 sasa inahuishwa japo kibarua bado kipo:Guterres
Safari ya malengo ya maendeleo endelevu au SDGs alianza mwaka 2015 na kila mtu anajua wapi ni mwisho wa safari yetu, kutokomeza umasikini na njaa, usawa kwa wanawake na wasichana , kuwawezesha vijana, kupunguza hewa ukaa, kuwa na uchumi wa kukabili mabadiliko ya tabianchi, ajira zenye hadi na mafanikio ya pamoja, jamii zenye amani na haki, haki za binadamu kwa wote na kuheshimu utawala wa sheria. Pia fursa kwa wote za kuishi katika dunia bora.
Mustakabali ni wa wazalendo na si wakumbatia utandawazi- Trump
Rais Donald Trump wa Marekani amehutubia mjadala mkuu wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa akipigia chepuo uzawa badala ya utandawazi.
Tutafanya kila tuwezalo kutimiza huduma za afya kwa wote:Sicily Kariuki
Ili serikali ya Kenya ifanikishe utimizaji wa malengo ya maendeleo endelevu au SDG’s ifikapo mwaka 2030 ni lazima huduma za afya kwa wote zipatikane kuhakikisha nguvu kazi imara ya kusongesha mbele mchakato huo, amesema waziri wa afya wa nchi hiyo.
Dunia imeghubikwa na zahma, hofu imekuwa ada:Guterres
Mjadala mkuu wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, UNGA74 umeanza leo kwenye makao makuu ya umoja huo jijini New York, Marekani ambapo Katibu Mkuu Antonio Guterres amesema kuwa hofu imetanda duniani hivi sasa na ni jukumu la viongozi kuondoa hofu hiyo miongoni mwa wananchi wao.
24 Septemba 2019
Hofu imegeuzwa mtaji hivi sasa duniani, Katibu Mkuu wa UN Antonio Guterres aueleza mjadala mkuu wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, UNGA74. Waziri wa afya wa Kenya Sicily Kariuki asema ili tutimize SDGs Kenya lazima tuhakikishe huduma za afya kwa wote. Naye Waziri wa fedha na mipango wa Tanzania Dkt Philip Mpango atoa wito kwa jumuiya ya kimataifa kushirikiana kutekeleza SDGs.