Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

MKUTANO WA 74 WA BARAZA KUU LA UMOJA WA MATAIFA

MKUTANO WA 74 WA BARAZA KUU LA UMOJA WA MATAIFA
MJADALA MKUU WA UNGA74

Mkutano wa 74 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa unaanza mwezi huu wa Septemba hadi wiki ya pili ya mwezi Septemba mwakani. Katika ukurasa huu hata hivyo tutakuwa tunakuletea habari motomoto kutoka mjadala wa wazi na vikao vya ngazi ya juu vya mkutano huo ambavyo vinafanyika kuanzia tarehe 22 septemba 2019 hadi 30 Septemba 2019. Pamoja na hotuba za viongozi ni vikao vya ngazi ya juu kuhusu  Mkutano wa vijana wa vijana na mabadiliko ya tabianchi, fursa ya afya kwa wote, mkutano kuhusu fursa ya afya kwa wote, tathimini ya hatua za utekelezaji wa malengo ya maendeleo endelevu, ufadhili kwa ajili ya maendeleo na tathimini ya mwelekeo wa mkakati wa SAMOA.

26 Septemba 2019

Wanawake wanahitajika zaidi katika tasnia ya ubaharia kama ilivyo tasnia nyingine, linasema shirika la kimataifa la shughuli za usafirishaji wa majini IMO. Elimu, ujumuishwaji na mabadiliko ya tabianchi ni baadhi vya vipaumbele vya Kenya asema Rais Uhuru Kenyatta. Na Profesa Antoine Kiamiantako Miyamueni, mdadhiri wa masuala ya uchumi katika chuo kikuu cha Kinshasa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ( DRC)  amesema ushirikiano baina ya vyuo vikuu utasaidia kuinua elimu Afrika.

Sauti
10'27"
Wenyeji wa Watamu, Kenya washirikiana na mamlaka kuondoa taka ya plastiki kutoka kwenye ufukwe wa bahari.
Cyril Villemain/UNEP

Elimu, ujumuishwaji na mabadiliko ya tabianchi ni baadhi vya vipaumbele vya Kenya:rais Kenyatta

Tumefika hapa kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa kuungana na nchi wanachama kuelezea ambayo Kenya imeyafanya katika kuhakikisha inaendana na vipaumbele vya mkutano huu wa Baraza Kuu la Umoja huo UNGA74 ikiwemo mabadiliko ya tabianchi, ujumuishwaji na ushirikiano wa kuhakisha utimizaji wa malengo ya maendeleo endelevu SDGs ifikapo mwaka 2030.

Sauti
2'4"
Mkakati wa FAO wa kusaidia kukabiliana na njaa kwenye bonde la Ziwa Chad umeleta nuru kwenye uhakika wa chakula.
FAO/Pius Utomi Ekpei

‘Mkono kwa mkono’ kunusuru njaa katika nchi maskini- FAO

Shirika la chakula na kilimo duniani, FAO limesema kitendo cha nchi wanachama wa Umoja waMataifa kusaidia na kuunga mkono harakati za shirika hilo kama mpango mpya wa Mkono kwa Mkono,  kitaasaidia kuchagiza mafanikio ya malengo ya maendeleo endelevu, SDGs hususan lile la kutokomeza njaa, na hivyo kutomwacha nyuma mtu yeyote.