Mkutano wa 74 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa unaanza mwezi huu wa Septemba hadi wiki ya pili ya mwezi Septemba mwakani. Katika ukurasa huu hata hivyo tutakuwa tunakuletea habari motomoto kutoka mjadala wa wazi na vikao vya ngazi ya juu vya mkutano huo ambavyo vinafanyika kuanzia tarehe 22 septemba 2019 hadi 30 Septemba 2019. Pamoja na hotuba za viongozi ni vikao vya ngazi ya juu kuhusu Mkutano wa vijana wa vijana na mabadiliko ya tabianchi, fursa ya afya kwa wote, mkutano kuhusu fursa ya afya kwa wote, tathimini ya hatua za utekelezaji wa malengo ya maendeleo endelevu, ufadhili kwa ajili ya maendeleo na tathimini ya mwelekeo wa mkakati wa SAMOA.
MKUTANO WA 74 WA BARAZA KUU LA UMOJA WA MATAIFA
Tufanye kazi na wanaoamini kwenye mabadiliko ya tabianchi- Kabudi
Mjadala Mkuu wa mkutano wa 74 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, UNGA74, ukiingia siku ya nne hii leo kwenye makao makuu ya umoja huo jijini New York, Marekani, Tanzania imesema imetenga asilimia 32 ya eneo la nchi kama hifadhi ya misitu kama njia mojawapo ya kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.
UN yatathimini hatua zilizopigwa mchakato wa SAMOA kuhusu visiwa vidogo vinavyoendelea
Wakuu wa nchi na viongozi wa serikali ni miongoni mwa waliokusanyika kwenye Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa leo Ijumaa Septemba 27 kushiriki mkutano maalum wa tathimini ya hatua zilizopigwa na nchi za visiwa vidogo zinazoendelea (SIDS) akiwemo Rais wa Ireland, Kenya na waziri mkuu wa Fiji na Norway.
Tanzania, Burundi na Kenya na ujumbe wao kwa Mkutano Mkuu wa Baraza Kuu la UN, UNGA74
Sasa ni mada kwa kina tukimulika kile ambacho Kenya, Burundi na Tanzia zimewasilisha mbele ya viongozi w anchi 193 wanachama wa Umoja wa Mataifa wakati wiki hii ya mjadala mkuu kwa lengo la kufanikisha ajenda ya maendeleo endelevu SDGs sambamba na amani, usalama na haki za binadamu.
Tusipoteze muda na wasioamini kwenye mabadiliko ya tabianchi- Tanzania
Mjadala Mkuu wa mkutano wa 74 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, UNGA74, ukiingia siku ya nne hii leo kwenye makao makuu ya umoja huo jijini New York, Marekani, Tanzania imesema imetenga asilimia 32 ya eneo la nchi kama hifadhi ya misitu kama njia mojawapo ya kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.
Mkutano wa Kiir na Machar umerejesha imani Sudan Kusini- Deng Gai
Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa hii leo limejulishwa kuwa mkutano kati ya Rais Salva Kiir wa Sudan Kusini na mpizani wake Riek Machar kwenye mji mkuu Juba hivi karibuni ulikuwa ni fursa pekee ya kutatua masuala muhimu ambayo hayajapatiwa ufumbuzi kwenye mzozo unaoendelea nchini humo.
Elimu, ujumuishwaji na mabadiliko ya tabianchi ni baadhi vya vipaumbele vya Kenya aeleza Rais Uhuru Kenyatta
Tumefika hapa kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa kuungana na nchi wanachama kuelezea ambayo Kenya imeyafanya katika kuhakikisha inaendana na vipaumbele vya mkutano huu wa Baraza Kuu la Umoja huo UNGA74 ikiwemo mabadiliko ya tabianchi, ujumuishwaji na ushirikiano wa kuhakisha utimizaji wa malengo ya maendeleo endelevu SDGs ifikapo mwaka 2030.
Dunia inahitaji madini, ajira za viwandani, mafunzo na maendeleo- rais Tshisekedi
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, DRC inauhitaji Ujumube wa Umoja wa Mataifa nchini DRC, MONUSCO lakini inahitaji MONUSCO iliyo haraka kutekeleza wajibu wake, ulio na vifaa, ulio thabiti na ambao una wajibu sahihi, amesema rais wa DRC, Felix Tshisekedi katika hotuba yake ya kwanza kwa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa Leo Alhamisi Septemba 26.
Ufadhili wa SDGs na mabadiliko ya tabianchi unademadema:UN
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ameonya mbele ya mjadala mkuu wa Umoja wa Mataifa kwamba kuna pengo kubwa la ufadhili ili kuweza kufikia malengo ya maendeleo endelevu SDGs na kukabiliana na dharura ya mabadiliko ya tabianchi.
Kutokomeza nyuklia ni kuachana nazo kabisa- Guterres
Njia pekee ya kutokomeza tishio la silaha za nyuklia duniani ni kuachana kabisa na silaha hizo, amesema Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres wakati akihutubia mkutano wa ngazi ya juu wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, kando mwa mjadala mkuu wa baraza hilo jijini New York, Marekani.